Loading...

Spika wa Bunge alikataa swali la Kubenea


SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amekalitaa swali la Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Ndugai ametoa uamuzi huo bungeni jijini Dodoma wakati wa kipindi cha maswali ya papo hapo kwa Waziri Mkuu.

Mbunge huyo wakati anauliza swali amesema, sera ya Serikali ni kuruhusu kila mtu aabudu dini anayotaka, kutoruhusu kuingilia dini ya mtu mwingine, na kwamba wananchi wana dini ila Serikali haina dini.

Amesema, Serikali imetoa kibali kwa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) pekee kuratibu hija ya mwaka huu kwa wanaokwenda kuhiji Mecca, Saudi Arabia na kwamba taasisi nyingine nyingine zilizokuwa zinafanya kazi kama hiyo zimezuiwa ikiwemo kamisheni ta Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar.

Kwa mujibu wa Mbunge huyo, uamuzi huo umesababisha sintofahamu ikiwa ni pamoja na ukubwa wa gharama zinazotozwa na Bakwata kulinganisha na taasisi nyingine hivyo alitaka kufahamu kama Serikali ipo tayari kuruhusu taasisi nyingine zipeleke mahujaji Mecca.

“Mheshimiwa Kubenea mbona kila ukisimama unauliza maswali ya kidini, yaani ukisimama una mambo ya kidini, ukisimama una mambo ya kidini” amesema Spika Ndugai.

Kubenea amesema anauliza swali hilo kwa kuwa anawakilisha Watanzania wakiwemo Waislamu, yeye pia ni Muislamu na ana maslahi kwenye jambo la hijja.

Baada ya kauli ya Mbunge huyo, Ndugai aliruhusu Mbunge Moses Mlata amuulize swali Waziri Mkuu akimaanisha kuwa amelikataa swali la Kubenea.
Spika wa Bunge alikataa swali la Kubenea Spika wa Bunge alikataa swali la Kubenea Reviewed by Zero Degree on 5/10/2018 01:48:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.