Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 10 Mei, 2018

Sergio Aguero
Mshambuliaji wa Manchester City, Sergio Aguero anaweza kurejea Atletico Madrid kuchukua nafasi ya Antoine Griezmann, ambaye anatarajiwa kwenda Barcelona. (Mundo Derpotivo)

Arsenal wamewasiliana na mawakala wa Layvin Kurzawa kuona kama beki huyo wa kushota anayeichezea PSG anaweza kuvutiwa na uhamisho kwenda Emirates. (RMC Sports)

Leroy Sane yuko tayari kufuata utaratibu wa Gabriel Jesus wa kucherewesha mazungumzo ya mkataba mpya na Manchester City hadi baada ya michuano ya Kombe la Dunia.

Marco Silva amekuwa akizungumziwa tena mara kadhaa kwenye chumba cha kubadilishia nguo cha Everton, hatima ya Sam Allardyce ikiwa shakani.

Leicester na Newcastle wanaweza kushindania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Hannover, Niclas Fullkrug.

Wolves wamemfanya kiungo wa klabu ya AC Milan, Andre Silva kuwa chaguo lao la kwanza kwenye usajili wa majira ya joto.

Bournemouth wanapanga kumsajili beki wa FC Porto ya Ureno, Diogo Queiros kwa pauni milioni 10.

Majeraha ya goti la James Maddison sio ya kutisha sana kama ilivyofikiriwa awali, kitu ambacho kinaweza kikachochea vita ya Tottenham, Arsenal na Manchester City kuwania saini ya kiungo huyo wa Norwich.

Wahbi Khazri
Sunderland wanaweza kumuuza Wahbi Khazri kwenda klabu ya Marseille kwa pauni milioni 6 baada ya kuonyesha uwezo wa kuvutia akiwa na Rennes kwa mkopo.

Crystal Palace imejiunga na orodha kubwa ya vilabu vinavyowania saini ya winga wa klabu ya Galatasaray, Garry Rodrigues. (Sun)

Stoke City wamejiandaa kwa pigo kwa Kevin Wimmer, ambaye anaweza kurejea Bundesliga mwaka mmoja baada ya uhamisho wake uliogharimu pauni milioni 18.

Stoke pia wanatarajiwa kumuuza kwa mkopo mshambuliaji Saido Berahino aliyesajiliwa kwa pauni milioni 12 na kumuuza Gianelli Imbula aliyesajiliwa kwa pauni milioni 18.

Southampton wataanzisha mazungumzo na Mark Hughes wiki ijayo kuhusiana na kusaini mkataba mpya mrefu kama meneja wa klabu hiyo. (Telegraph)

Arsenal wamemwondoa Luis Enrique kutoka kwenye orodha yao ya wagombea wa nafasi ya meneja mpya, orodha inayowajumuisha Max Allegri, Mikel Arteta, Patrick Vieira, Leonardo Jardim na Julian Nagelsmann.

Paris Saint-Germain wanakazania kumsajili beki wa klabu ya Fulham, Ryan Sessegnon mbele ya Man Utd, Tottenham na Man City.

Jack Wilshere anatarajiwa kuitumikia Arsenal kwa mkataba utakaoisha kwenye majira ya joto mwaka 2022.

Wilfried Kanon
Everton inaweza kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea kwenye mbio za kuwania saini ya beki kutoka Ivory Coast, Wilfried Kanon, ambaye anaichezea ADO Den Haag ya Uholanzi.

Manolo Gabbiadini anatarajiwa kuondoka Southampton kwenye majira ya joto licha ya kufunga goli lililoihakikishia klabu yeke kusalia kwenye Ligi Kuu ya Uingereza. (Mirror)

Wayne Rooney ameiambia Everton kuwa anataka kujiunga na DC United, huku dili la pauni milioni 12.5 likiwa njiani kukubaliwa.

Nafasi ya David Moyes kama meneja wa West Ham inaendelea kuwa shakani, huku akitarajia kupokea ofa nyingi kwenye majira ya joto.

Tottenham wanafuatilia maendeleo ya beki wa kati wa klabu ya Ajax, Matthijs de Ligt.

Steve McClaren anatarajiwa kuwa meneja mpya wa Queens Park Rangers, Ian Holloway akiwa hatarini kutimuliwao.

West Ham wamemchunguza nyota kutoka Ubelgiji, Leander Dendoncker lakini hawana uhakika kama thamani yake inafikia pauni 18m, ambazo zimetajwa na klabu yake ya Anderlecht.

Graham Alexander na John Sheridan ni miongoni wanaogombea nafasi ya kuwa meneja wa Salford City.

James McArthur
Klabu ya Cardiff City, ambayo imepanda daraja majuzi inavutiwa na kiungo wa Crystal Palace, James McArthur. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 10 Mei, 2018  Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 10 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/10/2018 10:40:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.