Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 19 Mei, 2018

Robert Lewandowski
Mshambuliaji wa klabu ya Bayern Munich, Robert Lewandowski anatafakari juu ya uhamisho kwenda Chelsea kwenye majira ya joto.

Lyon wanahofia nyota anayewindwa na klabu ya Liverpool, Nabil Fekir atakuwa anacheza mechi ya mwisho katika klabu hiyo wikendi hii dhidi ya Nice.

Thierry Henry atapewa kibarua cha ukufunzi katika klabu ya Arsenal kama sehemu ya benchi la ufundi la Mikel Arteta. (Express)

Wawakilishi wa kiungo wa Arsenal, Jack Wilshere wamemtoa nyota huyo kama ofa kwa klabu ya Paris Saint-Germain. 

Saint-Etienne wanataka kumsajili aliyekuwa kiungo wa Newcastle, Remmy Cabella anayeichezea Marseille licha ya kuwa na majeraha yatakayomweka nje ya Uwanja hadi mwanzoni mwa msimu ujao.  (L'Equipe)

David Moyes anashika nafasi ya kwanza kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya Paul Lambert kama meneja wa Stoke City.

Meneja wa Ostersunds, Graham Potter anaongoza mbio za kuwania nafasi ya Carlos Carvalhal katika klabu ya Swansea.

Mmiliki wa klabu ya Huddersfield, Dean Hoyle ana uhakika meneja wa klabu hiyo, David Wagner atasaini mkataba mpya na klabu hiyo.

Joe Hart
Wolves na Southampton zinaweza kumpa Joe Hart ofa ya itakayofuta machungu yake ya kukosa nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia kwa kumpa nafasi ya kubaki katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Aston Villa imekuwa ikimfuatilia mshambuliaji wa Porto, Moussa Marega katika maandalizi ya kurejea Ligi Kuu ya Uingereza.

Leeds imempa Tom Pearce ofa ya mkataba wa mpya wa miaka mitatu kumfanya asishawishike na kwenda kujiunga na vilabu vikubwa. (Mirror)

Benchi la ufundi itakayofanya kazi chini ya Mikel Arteta ndio limechelewesha Mhispania huyo kuthibitishwa kuwa mrithi wa Arsene Wenger kama meneja wa Arsenal. (Independent)

Leicester City wanalifanyia kazi dili la uhamisho wa pauni milioni 3 kumnasa beki wa klabu ya West Brom, Jonny Evans, lakini wataingia gharama za kulipia pauni miloni 4 za ziada kwa ajili ada ya wakala.

Chipukizi wa Chelsea, Mason Mount amealikwa kufanya mazoezi pamoja na kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kitakachoshiriki Kombe la Dunia kabla ya kwenda Urusi.

Wayne Rooney ana mwaliko wa kurejea Everton, endapo ataamua kukubali ofa ya kujiunga na DC United kumalizia maisha yake ya soka kama mchezaji kwenye Ligi Kuu ya Marekani, MLS. (Daily Mail)

Ruud Gullit amemtaja Roman Abramovich kuwa chanzo kikubwa kwa Chelsea kusindwa kufuzu Ligi ya Mabingwa, kwa sababu ya utaratibu wake wa kuajiri na kufukuza wakufunzi.

Eden Hazard
Manchester City watafanya usajili wa kusisimua kwa kumnasa Eden Hazard kwenye majira ya joto kama Mbelgiji huyo ataamua kuondoka Chelsea.

Southampton wanatarajiwa kutoa ofa ya pauni milioni 20 kumnasa beki wa klabu ya Middlesbrough, Ben Gibson.

Chris Coleman anatazamia kurejea kwenye kibarua cha ukufunzi kwa kasi kubwa baada ya Swansea kumfuta kazi Carlos Carvalhal. (Sun)

Marco Silva atafanya mazungumzo zaidi na klabu ya Everton wiki ijayo juu ya nafasi ya meneja iliyoachwa wazi na Sam Allardayce.

Mick McCarthy ameiambia klabu ya Stoke City kuwa ana nia ya kuichukua nafasi ya Paul Lambert kama meneja. (Telegraph)

Aliyekuwa meneja wa Crystal Palace, Frank de Boer na meneja wa Ostersunds, Graham Potter ni vinara kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya ukufunzi katika klabu ya Swansea. (Guardian)

Mwenyekiti msaidizi wa klabu ya West Ham, Karren Brady alipendekeza kwamba klabu hiyo izungumze na meneja wa Burnley, Sean Dyche kuhusiana na nafasi ya kazi ya umeneja. (Times)

Brighton wanakaribia kukamilisha dili la kumsajili mshambuliaji wa klabu ya Deportivo La Coruna, Florin Andone. (Star)

Martin Skrtel
Fenerbahce wataifanya klabu ya Rangers iendelee kusubiri licha kuwa na hamu ya ofa ya pauni milioni 4 iliyoripotiwa kutolewa na klabu hiyo ya Uskoti kwa ajili ya aliyekuwa beki wa klabu ya Liverpool, Martin Skrtel. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 19 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumamosi Tarehe 19 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/19/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.