Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 8 Mei, 2018
Cristiano Ronaldo |
Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amethibitisha kuwa Cristiano Ronaldo atakuwa 'fiti' kuikabili Liverpool kwenye fainali ya Ligi ya Mabingwa.
Rafael Benitez anataka kuwasajili moja kwa moja Kenedy na Martin Dubravka, ambao waitumikia klabu ya Newcastle kwa mkopo. (Sky Sports)
Mmiliki wa klabu ya Bristol City, Steve Lansdown anataka Lee Johnson aendelee kuwa meneja wa klabu hiyo, huku West Brom ikiwa na nia ya kumpa kibarua.
Ipswich wanatafakari juu ya kumtangaza Tim Sherwood kuwa meneja wao mpya. (Star)
Wachezaji wa Tottenham watakosa malupulupu yao kama wataipoteza nafasi ya kushiriki Ligi ya Mabingwa.
Dili la Shahid Khan kuununua Uwanja wa Wembley limesimamishwa kwanza, kwa lengo la kuwashirikisha wananchi watoe maoni yao. (Daily Mail)
Juventus wameulizia uwezekano wa kumsajili mshambuliaji wa Chelsea, Alvaro Morata, na wanawezza kutumia kiasi cha pauni milioni 60 kumnasa Mhispania huyo ambaye amekuwa na wakati mgumu katika msimu wake wa kwanza.
Lewis Dunk |
Beki wa klabu ya Brighton, Lewis Dunk anasubiria kuona kama mabadiliko ya uongozi katika klabu ya Arsenal yatasitisha nia yao ya kutaka kumsajili.
Klabu ya Ajax inavutiwa na huduma ya kiungo wa timu ya taifa ya Croatia na Southampton, Dusan Tadic.
Golikipa wa Burnley, Tom Heaton anahofia kukosa nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia 2018 kwa sababu ya ukosefu wa muda wa kutosha uwanjani.
Sam Allardyce anasistiza kuwa Everton iko njiani kuelekea nne bora baada ya mabadiliko makubwa Goodison Park.
Rafa Benitez anataka mikakati ya usajili katika klabu ya Newcastle ipangwe wiki hii - na kusema hataielewa klabu kama itashindwa kupambana kwenye soko la usajili wa wachezaji.
Dean Marney anaweza kutimkia Nottingham Forest baada ya miaka nane katika klabu ya Burnley. (Mirror)
Arsene Wenger anatazamia kibarua kingine cha ukufunzi chenye mkatab wa muda mrefu baada ya kuondoka Arsenal.
Ligi Kuu ya Uingereza inaandaa ratiba ili timu "sita bora" za juu zikutane wikendi za kwanza au za mwisho wa msimu.
Michail Antonio |
Meneja wa Crystal Palace, Roy Hodgson amemuongeza mshambuliaji wa West Ham, Michail Antonio kwenye orodha ya wachezaji anaowataka kwenye usajili wa majira ya joto. (Times)
Arsenal inaendelea vizuri na mazungumzo ya kumbakisha Jack Wilshere - licha ya uwepo wa ofa kubwa kutoka Wolves.
Hatima ya David Moyes katika klabu ya West Ham inabakia kuwa hewani, huku pande zote mbili zikikosa uhakika wa mkataba wa kudumu. (Telegraph)
Kuondoka kwa Emre Can katika klabu ya Liverpool kunaweza kutoa wasaa kwa klabu hiyo kumsajili Sami Khedira kutoka Juventus.
West Ham, Newcastle na Swansea ni miongoni mwa vilabu vinavyoshindania saini ya Joe Allen, ambaye anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 20 baada ya Stoke City kushuka daraja.
Newcastle wanaripotiwa kuwa kwenye ushindani na klabu ya Tottenham pamoja na Wolves kuwania saini ya beki wa Southampton, Ryan Bertrand.
Artur Boruc anatarajia kupewa mkataba mpya wa mwaka mmoja katika klabu ya Bournemouth, ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo hadi katika umri wa miaka 39.
Phil Parkinson anahofia kutemwa na Bolton, huku klabu hiyo ikiwa mbioni kuuzwa kwa kundi moja la Wasaudia. (Sun)
Yoshinori Muto |
West Ham wanamchunguza mshambuliaji wa Mainz, Yoshinori Muto, ambaye goli lake la wikendi iliyopita lilisaidia kuiepusha klabu yake na kushuka daraja Bundesliga. (Express)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 8 Mei, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
5/08/2018 11:05:00 AM
Rating: