Loading...

"Tumetoka kwa utata" - Sugu


Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ' Sugu' ameweka wazi kwamba waliingizwa Magereza kwa utata na wametoka kwa utata jambo ambalo amewapa pole wananchi wa jimbo lake akidai kuwa nao walikuwa kifungoni.

Mbunge huyo ameyasema hayo leo wakati akizungumza na wanahabari pamoja na wananchi wa jimbo lake baada ya kuachiwa huru kutoka katika gereza la Ruanda alikokuwa akitumikia kifungo cha miezi mitano yeye pamoja na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyassa, Emmanuel Masonga.

Mh. Sugu amesema kwamba anawapa pole wanambeya kwani anaamini walifungwa mioyo pamoja na kisaikolojia jambo ambalo ni baya sana.

"Tumetumikia kifungo cha miezi mitano mpaka siku ya leo ambayo tumetoka katika mazingira haya tuliyotoka ambayo sisi tunasema tuliingia kwa utata na tumetoka kwa utata."

Kwa upande wake Masonga amesema kwamba kama jinsi ambavyo walivyoingia magereza kiholela wametoka kiholela kwani hawaelewi ni kwa namna gani hesabu zimetumika kuweza kuwatoa magereza siku ya leo na ndiyo maana awali walisema kuwa wamepelekwa gerezani kwa hila.

Source: EATV
"Tumetoka kwa utata" - Sugu "Tumetoka kwa utata" - Sugu Reviewed by Zero Degree on 5/10/2018 02:53:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.