Loading...

Mapato ya viingilio Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA)


MCHEZO wa fainali Kombe la Shirikisho la Azam (FA) ulizozikutanisha timu ya Mtibwa Sugar na Singida United, uliingiza mapato ya uwanjani ya Sh milioni 20 mchezo uliopigwa mwishoni mwa wiki kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini hapa.

Mashabiki wa soka walifurika kushuhudia mtanange huo kutoka maeneo mbalimbali ya ndani na nje ya mkoa Arusha, ambao Mtibwa Sugar waliibuka na ushindi dhidi ya Singida United ya Singida. Taarifa iliyotolewa na Chama cha Soka mkoa Arusha (ARFA), kupitia kwa mwenyekiti wake Peter Temu ilieleza kuwa mchezo huo uliwakutanisha jumla ya watazamaji 11,400 waliokata tiketi na kuingia uwanjani wakati uwanja huo unabeba watazamaji 12,000.

Kutokana na mapato hayo, serikali ilifaidika kupitia kodi ya VAT kwa mgao wa Sh 3,050,847.46, wakati gharama ya tiketi ilikuwa Sh 2,622,000.00, huku wamiliki wa uwanja, ambao ni Chama cha Mapinduzi (CCM, waliondoka na Sh 2,149,072.88, Timu ya Mtibwa Sugar FC ilipata 3,581,788.14 sawa na wenzao wa Singida United. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) lenyewe liliondoka na Sh 2,865,430,

Baraza la Michezo Tanzania (BMT) 143,271.53, wakati gharama za mchezo ilikuwa sh 1,289,443.73 na Chama cha Soka mkoa wa Arusha (ARFA) kilipata 716,357.63 kufanya jumla ya jumla ya Sh 20,000,000 kwa idadi ya watazamaji 11,400. Ikumbukwe kuwa viingilio katika mchezo huo vilikuwa bwerere, ambapo jukwaa kuuu (VIP A) ilikuwa ni Sh 10,000, jukwaa B1 na B2 Sh 2,000 na jukwaa C, ambalo ni mzunguko, watazamaji walilipa Sh 1,000 kwa kichwa.

Mchezo huo wa fainali ulimalizika kwa timu ya Mtibwa kuibuka mabingwa baada ya kuichakaza Singida United kwa mabao 3-2 na kupata nafasi ya kuliwakilisha taifa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho.
Mapato ya viingilio Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) Mapato ya viingilio Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) Reviewed by Zero Degree on 6/06/2018 06:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.