Loading...

Fabregas ndani ya Rekodi za Guinness kwa kufikisha 'assist' 100 EPL


Cesc Fabregas ameingia kwenye Rekodi za dunia za Guinness kwa kuwa mchezaji aliyefikisha assist 100 kwa kutumia muda mfupi zaidi kwenye Ligi Kuu ya Uingereza, EPL.

Kiungo huyo wa klabu ya Chelsea alifikisha ilifikia rekodi hiyo alipo toa assist na kumsaidia Wilian kuiandikia Chelsea bao la nne dhidi ya Stoke tar 31 Disemba, 2016.




Fabregas alifikisha rekodi hiyo ya assist 100 ndani ya michezo 293, mechi 74 mbele ya Ryan Giggs ambaye alifikisha idaid hiyo ndani ya michezo 367.

"Mimi sio mchezaji mwenye kasi zaidi, sio mwenye nguvu zaidi, sio mwepesi zaidi na sio kwamba naweza kuruka juu zaidi
 kuliko wengine," alisema beki huyo wa zamani wa klabu ya Arsenal.

"Lakini kufikia rekodi hii kwenye soka ni moja ya vitu vya kujivunia zaidi katika hii kazi yangu, kwa sababu ni kazi yangu na nimeanya vizuri."
Fabregas ndani ya Rekodi za Guinness kwa kufikisha 'assist' 100 EPL Fabregas ndani ya Rekodi za Guinness kwa kufikisha 'assist' 100 EPL Reviewed by Zero Degree on 10/17/2018 02:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.