Radi yaua wanafunzi 6 Geita, 25 wajeruhiwa
Ofisa Elimu Msingi wilayani Geita, Yese Kanyuma, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema mvua kubwa iliyoambatana na radi imenyesha leo asubuhi na kusababisha madhara hayo.
“Tukio hilo la radi limetokea majira ya saa 3 asubuhi na kusababisha vifo vya wanafunzi sita wa darasa la pili na la tatu, wengine 25 wamejeruhiwa lakini wanaendelea na matibabu wodini. Tunawashukuru madaktari na wauguzi kwa jitihada zao kuokoa maisha ya watoto hao waliojeruhiwa,” amesema Kanyuma.
Radi yaua wanafunzi 6 Geita, 25 wajeruhiwa
Reviewed by Zero Degree
on
10/17/2018 01:15:00 PM
Rating: