Loading...

Tanzania ni ya 12 kwa uzalishaji wa muhogo duniani


TANZANIA ni nchi ya 12 katika uzalishaji muhogo duniani na ya sita barani Afrika baada ya Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC), Ghana, Angola na Msumbiji.

Akifungua mkutano ya siku tatu wa wadau wa sekta ya muhogo wakiwemo watunga sera, watafiti, sekta binafsi na wakulima waliokutana jijini hapa, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kilimo, Profesa Siza Tumbo alisema muhogo ni zao la pili kwa umuhimu likitanguliwa na mahindi.

Profesa Tumbo alisema uzalishaji wa muhogo nchini, kila mwaka unachangia asilimia 5.5. ya uzalishaji wa muhogo duniani na asilimia 14 ya uzalishaji Afrika. Profesa huyo alisema mahitaji ya baadaye ya muhogo nchini, yataongeza uzalishaji na kuwa kati ya tani 530,000 na 630,000, hali hiyo inachangiwa na kuongeza thamani ya muhogo.

“Thamani ya muhogo inaongezeka kutokana na kutengeneza unga, wanga na kuwa malighafi katika viwanda vya bia, pipi na vitafunio, viwanda vya nguo, karatasi na mbaongumu, rangi na dawa,” alisema.

Mkutano huo umeandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Taasisi ya Kimataifa ya Kitropiki (IITA) na Wizara ya Kilimo, Kitengo cha Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Kilimo Awamu ya Pili (ASDP), unalenga kuhimiza wadau kuongeza uzalishaji zao hilo.

Alisema asilimia 84 ya uzalishaji nchini ni kwa matumizi ya chakula cha binadamu, lakini uzalishaji wake bado upo chini na zao hili halijatumika kikamifu. “Ninawahimiza washiriki kuendeleza hatua ya kukubiliana na changamoto ambazo zimekuwa zikikabili jitihada za kufanya muhogo kuwa zao la biashara ili kuboresha mapato ya wakulima wadogo na kusaidia nchi yetu kuelekea kufikia Dira ya Maendeleo ya 2025,” alisema.
Tanzania ni ya 12 kwa uzalishaji wa muhogo duniani Tanzania ni ya 12 kwa uzalishaji wa muhogo duniani Reviewed by Zero Degree on 10/17/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.