Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Octoba, 2018

Mauro Icard
Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde amesema kuwa klabu hiyo inaweza kumrejesha Mauro Icard Nou Camp.

Kumfuta meneja Julen Lopetegui, 52, kunaweza kuigharimu Real Madrid euro milioni 18. (Sport)

Lopetegui atafutwa na meneja wa akiba Santiago Solari, 42, achukue mahala pake kabla ya mechi ya Jumapili ya El Clasico dhidi ya Barcelona.

Kocha wa Togo Claude Le Roy amemuunga mkono mshambuliaji wa Liverpool na Senegal Sadio Mane 26, kuhamia klabu ya Manchester United. (Star)

Kocha wa Chelsea Marco Ianni, anayechukuliwa hatua na FA kwa kuhusika katika mzozo ya kuvuka mstari wakati upande wake ulitoka sare ya 2-2 na Manchester United, huenda akachukuliwa hatua zaidi baada ya kuibuka kuwa hata hakustahili kuwa katika eneo la kiufundi.

Ryan Sessegnon
Fulham wanatarajiwa kuanza mazungumzo ya mkataba na mlinzi mwenye miaka 18, Ryan Sessegnon, ambaye amekuwa akilengwa sana na Tottenham, ambaye amebaki na miezi 18 mkataba wake wa sasa kukamilika.

Chelsea watafikiria kumsaini mchezaji wa Genoa mshambuliaji, ambaye ni raia wa Poland, Krzysztof Piatek, 23, mwezi Januari.

Mmiliki wa klabu ya Nottingham Forest Evangelos Marinakis alisafiri kutoka Athens kupeleka ujumbe kuwa matokeo yao ni lazima yaimarike baada ya kushindwa kwa mara ya kwanza katika mechi saba. (Daily Mail)

Aliyekuwa kocha wa Uhuspania Lopetegui bado atasimamia El Clasico. (Mundo Deportivo)

Beki Mhispania Marcos Alonso, 27, amesaini mkataba mpya na Chelsea ambao utadumu hadi Juni 2023. (ESPN)

Mshambuliaji wa Inter Milan Mauro Icardi, 25, anasema hana nia ya kuondoka klabu ya Serie A. (AS)

Mlinzi wa Tottenham na Ubelgiji Toby Alderweireld, 29 amefichua kuwa atakuwa tayari kujiunga tena na klabu ya zamani Ajax siku za usoni. (Sky Sports)

Victor Moses
Winga raia wa Nigeria, Victor Moses, 27 yuko tayari kuondoka Chelsea, huku akiwa na wakati mgumu kupata nafasi ya kucheza chini ya umeneja wa Maurizio Sarri. (Goal)

Antonio Conte yuko juu zaidi ya orodha ya Real Madrid kuwa meneja wao mpya ikiwa watamfuta Julen Lopetegui, lakini hilo litafikisha kikomo fursa ya kumsaini Eden Hazard ambaye alikuwa na uhusiano mbaya na Muitalia huyo huko Chelsea. (Mirror)
Nyota ambaye klabu ya Chelsea inalenga kumsajili anawindwa pia na Juventus ya ligi kuu ya Italia.
 
Mlinzi wa Inter Milan raia wa Slovakia Milan Skriniar, 23, ambaye amehusishwa na Manchester United na Manchester City, bado hajakubaliana na mkataba mpya na klabu hiyo ya Italia. (Calciomercato)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Octoba, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 24 Octoba, 2018 Reviewed by Zero Degree on 10/24/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.