Aliyempa mimba dada yake ahukumiwa miaka 30 jela
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Misungwi, Erick Marley akisoma hukumu hiyo juzi alisema amechukua maamuzi hayo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka.
Akitoa ushahidi mahakamani hapo, Mwanafunzi huyo aliiambia mahakama kwamba mnamo Juni 6 saa 1:30 usiku akiwa chumbani kwake aliingiliwa na kubakwa na kaka yake (Charles Abel) ambaye ni mtoto wa baba yake mkubwa.
Mshtakiwa akijijitetea mahakamani hapo, aliomba kupunguziwa adhabu akidai kuwa hawezi kufanya mapenzi na dada yake na kwamba ametengenezewa kesi hiyo .
Hakimu Marley alisema Mahakama inamhukumu mshtakiwa kwa kosa la kwanza la ubakaji kifungo miaka 30 jela na kwamba, shtaka la pili la kumpa mimba mwanafunzi atatumikia miaka 30 jela, huku akieleza kuwa sababu adhabu zote zinakwenda pamoja atatumikia miaka 30 tu badala ya miaka 60.
Source: Mwananchi
Aliyempa mimba dada yake ahukumiwa miaka 30 jela
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2018 12:31:00 PM
Rating: