Mke wa mchungaji ajinyonga kanisani
Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo, Selina Kayange, alisema kuwa, mwanamke huyo anadaiwa siku za hivi karibuni alijifungua mtoto ambaye alifariki dunia.
Alisema baada ya mtoto huyo kuzikwa, bado mwanamke huyo alikuwa akienda makaburini kila siku ambako alikuwa akilia.
Hata hivyo, wiki iliyopita alitoweka nyumbani kwake na kuanza kusakwa kila mahali, ambapo jana mwili wake ulikutwa ndani ya kanisa huku akiwa ananing’inia kwa kujinyonga kwa kamba.
“Kitendo cha kuchukua uamuzi wa kujinyonga kwa kweli ni jambo gumu sana na lisilompendeza Mungu. Ni tukio ambalo limetushangaza sana, hivi kweli mke wa mchungaji unafikia hatua hii nzito, hapana hakustahili kufanya hivyo,” alisema Kayange.
Akizungumzia tukio hilo jana, Ofisa Mtendaji wa Kata ya Ngulilo, Nickodemas Yanga, alikiri kuwepo kwa tukio hilo na kusema kuwa alipata taarifa kutoka kwa uongozi wa kijiji, naye alitoa taarifa kwa uongozi wa wilaya ambao walifika katika eneo hilo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na kuchukua mwili huo kwa uchunguzi.

Source: Mtanzania
Mke wa mchungaji ajinyonga kanisani
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2018 11:58:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2018 11:58:00 AM
Rating: