Loading...

Amber Rutty, James Delicious wafikishwa mahakamani


Video queen wa Bongo Fleva, Ruth Abubakar ‘Amber Rutty’, mpenzi wake na mwanaume anayetuhumiwa kujihusisha na ushoga, James Delicious wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, – Dar, leo Ijumaa, Novemba 2, ili kusomewa mashtaka yanayowakabili.
Amber Ruty na mpenzi wake wanatuhumiwa kufanya ngono kinyume cha maumbile na kusambaza picha/video za kwenye mitandao ya kijamii na James Delicious anatuhumiwa kujihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja (ushoga).

Amber Rutty ambaye amefikishwa Mahakamani hapo akiwa anachechemea na kushindwa kukaa hadi alipopatiwa huduma ya kwanza na askari, pamoja na mpenzi wake wamesomewa mashtaka matatu, moja la kufanya mapenzi kinyume na maumbile, shtaka la pili ni kurekodi video za ngono na shtaka la tatu ni kusababisha kusambaa kwa picha na video za ngono kupitia mtandao wa WhatsApp.

“Hata hivyo watuhumiwa wamerudishwa rumande baada ya kushindwa kukidhi masharti ya dhamana ambayo walitakiwa kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini bondi ya Tsh. Milioni 15 kila mmoja.

Wakati huo huo kijana anayejulikana kwa jina la James delicious naye amepandishwa mahakamani na kusomewa shtaka moja la kusambaza video za ngono mtandaoni, ambapo amekana shtaka hilo.

Ifahamike kuwa iwapo watuhumiwa hao watakutwa na hatia juu ya makosa yao, kwa mujibu wa sheria za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watalazimika kwenda jela maisha au adhabu isiyopungua miaka 30 jela.
Amber Rutty, James Delicious wafikishwa mahakamani Amber Rutty, James Delicious wafikishwa mahakamani Reviewed by Zero Degree on 11/02/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.