Loading...

Nyota Real Madrid ataja nani ni bora kati ya Ronaldo na Cristiano Ronaldo

Kutoka kushoto, Zinedine Zidane, Ronaldo na Luis Figo, Real Madrid
Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno, Luis Figo anafikiri kwamba Mbrazil Ronaldo ana ufundi mwingi sana afikapo golini ukimlinganisha na Cristiano Ronaldo. Figo alisema pia kwamba Cristiano Ronaldo yuko vizuri sana kwa mipira ya vichwa.

Luis Figo na Cristiano Ronaldo, Ureno
Figo alicheza pamoja na Ronaldo De Lima katika klabu ya Real Madrid kwa muda wa miaka mitatu na miaka mitatu tena akiwa na Cristiano Ronaldo kwenye timu ya taifa ya Ureno. Alipoulizwa nani ni bora , Figo alisema, “Inategemeana, Cristiano anafunga magoli mengi kwa kichwa lakini kiujumla wote wana kipaji cha kuvutia. Kwa vile Cristiano Ronaldo bado anaendelea kucheza nitasema Ronaldo ni namba moja mbele ya goli, lakini kama nilivyosema, wote ni wachezaji ambao unaweza kuwatuma kusaka ushindi na wakatenda ipasavyo.

Jambo la msingi ni kuwaweka kwenye nafasi ya kufunga, kisha wao watamaliza kazi iliyobaki…”

Cristiano Ronaldo amekuwa kwenye kiwango cha kawaida akiwa na Juventus msimu huu na wengi wanategemea ataisaidia Juventus kushinda Taji la Ligi ya Mabingwa mwishoni mwa msimu huu.
Nyota Real Madrid ataja nani ni bora kati ya Ronaldo na Cristiano Ronaldo Nyota Real Madrid ataja nani ni bora kati ya Ronaldo na Cristiano Ronaldo Reviewed by Zero Degree on 11/02/2018 11:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.