Samatta aendeleza moto wa Europa kwenye Ligi Kuu ya Ubelgiji
Mbwana Ally Samatta |
Katika mchezo huo, Samatta alifunga mabao yake dakika za 76 na 90, baada ya kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy kutangulia kuifungia Genk mabao mawili dakika za 56 na 60 na yote kwa penalti, ambapo sasa amefunga jumla ya mabao 10 yanayomfanya kuwa kinara wa upachikaji mabao katika ligi hiyo.
Pia Samatta jana amefikisha mechi ya 126 katika mashindano yote tangu amejiunga na Genk Januari mwaka 2016 akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na amefunga jumla ya mabao 50.
Katika Ligi ya Ubelgiji amecheza mechi 98 na kufunga mabao 36, Kombe la Ubelgiji mechi nane mabao mawili na Europa League mechi 20 mabao 14.
Klabu ya Genk hivi sasa inaongoza ligi hiyo kwa jumla ya alama 33 Genk baada ya kucheza michezo 13, ikishinda mechi 10 na kutoka sare mechi 3 huku ikiwa haijapoteza mchezo wowote. Nafasi ya pili inashikiliwa na Club Brugge yenye alama 33 huku nafasi ya tatu na ya nne zikishikiliwa na Royal Antwerp pamoja na Anderlecht.

Reviewed by Zero Degree
on
11/01/2018 11:05:00 AM
Rating: