Yanga watoa tamko hili baada ya Banka kufungiwa
Kwa mujibu wa TFF kupitia Ofisa Habari wake, Clifford Mario Ndimbo, alieleza kuwa Banka mpaka sasa ni mchezaji wa Mtibwa Sugar kutokana na Yanga kushindwa kukamilisha taratibu za usajili wake.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya Banka kupitia Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Afrika (RADO) kutangaza kumfungia mchezaji huyo kwa muda wa miezi 14, kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi.
Licha ya maamuzi ya kifungo kutolewa na kauli hiyo, Ten amefunguka kwa kusema inashangaza shirikisho hilo kutamka maneno hayo akisema walifuata taratibu za usajili kwa mfumo mpya wa TFF FIFA CONNECT.
Ten amesema ukiingia katika mfumo huo mpya, unaonesha kuwa Banka ni mchezaji wa Yanga na akisema walizungumza na Mtibwa mapema kabla ya usajili kufanyika.
Aidha, Ten ameeleza watatoa maelezo zaidi wakishapokea barua rasmi ya kufungiwa kwa mchezaji wao ambaye waliamini alikuwa na ndoto za kufanya vema msimu huu akiwa na wachezaji wenzake ndani ya uwanja.
Mnamo Disemba 9, 2017 Mchezaji huyo akiwa Machakos nchini Kenya alichukuliwa vipimo vya mkojo ambavyo vilisafirishwa kwenda kwenye Maabara ya WADA iliyopo Doha, Qatar kwa uchunguzi zaidi na majibu kurudi yakiwa na tuhuma hizo zinazomkabili.

Reviewed by Zero Degree
on
11/01/2018 10:50:00 AM
Rating: