Ripoti: Tanzania, Rwanda vinara vita ya rushwa
Shirika la Kimataifa la Transparency International (TI), limetoa ripoti inayoonyesha hali ya ufisadi duniani kwa mwaka 2018.
Huku nchi za Tanzania na Rwanda zikiorodheshwa kwamba zimefanya vizuri katika vita dhidi ya rushwa.
Rwanda ilitajwa kufanya vizuri zaidi kwa kuwa na pointi 56 ikiwa katika nafasi ya 48 wakati Tanzania ikiwa katika nafasi ya 99 kwa kupata pointi 36.
Ripoti hiyo pia imebaini kuwa Kenya ilishuka kwa pointi moja tangu 2017, ambapo ilikuwa na pointi 28, huku mwaka jana ikiwa na pointi 27 na kushika nafasi ya 144 kati ya nchi 180.
Uganda imepata pointi 26 na kuchukua nafasi ya 149. Burundi iko katika nafasi ya 170 huku Sudan ikiwa katika nafasi ya 172 ikiwa na pointi 16 wakati ndugu zao wa Sudan Kusini wakiwa nafasi ya 178 na pointi 13.
Transparency International hutumia vigezo ambapo sifuri ni alama ya nchi inayofanya vizuri zaidi huku mia moja ikiwa ndiyo nchi iliyozorota zaidi katika nyanja hiyo.
Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Ferreira Rubia, alisema kuwa jinsi demokrasia ilivyokita mizizi kwa baadhi ya nchi, ndivyo uwezekano wa nchi hiyo kufanya vyema katika orodha hiyo ya nchi fisadi zaidi duniani.
Hata hivyo, nchi kama Marekani, ambayo hutajwa kama iliyoimarika kidemokrasia, pia ilishuka rekodi yake kutoka ilivyokuwa mwaka wa 2017.
Hizi ni nchi ambazo zimekuwa katika vita vya aina moja au nyingine, ikiwa ni ishara kwamba misukosuko ya ndani ya nchi inaathiri sana vita dhidi ya ufisadi, alisema mchambuzi wa masuala ya uchumi, Chrispus Yankeem katika mahojiano ya simu na Sauti ya Amerika.

Chanzo: Mwananchi
Ripoti: Tanzania, Rwanda vinara vita ya rushwa
Reviewed by Zero Degree
on
1/30/2019 11:35:00 AM
Rating: