Waitara: Tayari tumepata kibali cha kuajiri walimu 6000
Naibu Waziri, Mwita Waitara |
Akilijibu swali lililoulizwa na Mbunge wa Handeni, Omari Abdallah Kigoda, ameuliza, "swala la elimu bure limeleta changamoto kubwa , wanafunzi wengi wamejiandikisha lakini kuna uhaba mkubwa wa walimu, serikali ina mkakati gani kuajiri waalimu ili ipatikane elimu bora?"
Mh. Waitara amesema kwamba anafahamu elimu bure imeleta chachu na muamko, amesema kwamba sekondari kuna waalimu elfu 11 hivyo mzigo wao siyo mkubwa ndiyo maana wameomba washushwe.
Ameongeza kwamba changamoto iliyokuwepo awali ilitokana na kuwa wapo wale waalimu waliostaafu na wale waliodhibiwa kwa makosa mbalimbali na waliofariki hivyo ule mkwamo uliokuwa unazuia tayari Rais ameshauondoa na wataanza kuajiri kila mwaka ili kuweza kupunguza tatizo la walimu.
Mbali na hayo, Mheshimiwa Waitara amefafanua kwamba, "tayari tumepata kibali cha kuajiri walimu 6000 naamini watasaidia kupunguza changamoto katika shule za msingi na sekondari."
Waitara: Tayari tumepata kibali cha kuajiri walimu 6000
Reviewed by Zero Degree
on
1/29/2019 11:50:00 AM
Rating: