Loading...

Mwili waopolewa kwenye mabaiki ya ndege iliyoanguka

Emiliano Sala (kushoto) alikuwa ameabiri ndege iliyokuwa ikiendeshwa na David David Ibbotson

Mwili umeopolewa kutoka kwenye mabaki ya ndege iliyoanguka ikiwa imembeba mchezaji soka wa timu ya Cardiff City, Emiliano Sala na rubani David Ibbotson.

Kikosi cha uchunguzi wa ajali ya ndege kimeeleza kwamba wakandarasi maalum wamejiunga katika operesheni hiyo, katika 'hali yenye changamoto nyingi'.

Imefanyika 'kwa heshima kubwa iwezekanavyo' na familia za wote wawili ziliarifiwa kadri shughuli zilivyokuwa zikiendelea.

Mabaki ya ndege hiyo, iliyopotea wiki mbili zilizopita, yalipatikana kutoka huko Guernsey.

Ndege hiyo chapa Piper Malibu N264DB ilikuwa ikielekea kutoka Ufaransa kwenda Cardiff, baada ya mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 raia wa Argentina kurudi kwa safari ya haraka katika klabu yake ya zamani Nantes siku mbili baada ya kutangazwa kuidhinishwa kwa mkataba wake wa thamani ya £15m kwenda Cardiff .

Ibbotson, mwenye umri wa miaka 59, kutoka Crowle, Lincolnshire kaskazini, alikuwa kwenye mawasiliano na waongoza ndege ardhini ndege hiyo ilipokatiza mawasiliano na kupotea kwenye rada mnamo Januari 21.

Mashabiki wa Cardiff wakiwaweka mashada ya maua wakimuombea kheri Emiliano Sala

Shughuli rasmi ya kuisaka ndege hiyo ilisitishwa Januari 24 baada ya mamlaka kudai uwezekano wa kupatikana hai wawili hao ulikuwa "mdogo mno".

Hata hivyo, mabaki ya ndege hiyo yalipatikana chini ya bahari baada ya wasamaria wema kuchangisha fedha zilizowezesha operesheni ya binafsi iliyoongozwa na mwanasayansi ya bahari David Mearns.

Mashabiki wa Nantes pia wamekuwa wakimkumbuka Sala

Juhudi za kuinyanyua ndege hiyo toka chini ya bahari zimeshindikana kwa sasa kutokana na hali mbaya ya hewa.

Mwili huo ulioopolewa bado haujawekwa wazi kuwa ni wa nani kati ya Sala ama rubani na kwa sasa unapelekwa kwa mchunguzi wa mji wa Dorset.

Chanzo: BBC
Mwili waopolewa kwenye mabaiki ya ndege iliyoanguka Mwili waopolewa kwenye mabaiki ya ndege iliyoanguka Reviewed by Zero Degree on 2/07/2019 12:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.