Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Februari 1, 2019


Mlinzi wa Chelsea raia wa Uingereza Gary Cahill, 33, amekataa ofa za dakika ya mwisho kujiunga na klabu za Juventus, Monaco na Fulham.

Southampton wamekataa ofa ya vilabu vinne vya ligi kuu ya England ya kumsajili kwa mkopo mshambuliaji wake Charlie Austin, 29. (Sky Sports)

Meneja wa Blues Maurizio Sarri amekataa kusafiri katika basi moja na timu yake baada ya kupokea kipigo cha 4-0 kutoka kwa Bournemouth siku ya Jumatano. (Mail)

Barcelona yasajili nyota wa Brazil chini ya miaka 20, Emerson kwa dau la euro milioni 12.

Klabu ya Fulham imemsajili Markovic kutoka Liverpool. (ESPN)

Crystal Palace yasajili mshambuliaji wa klabu ya Chelsea, Michy Batshuayi kwa mkopo hadi mwisho wa msimu.

Klabu ya Arsenal imefanikiwa kummsajili Denis Suarez kwa mkopo kutoka Barcelona. (talkSport)

Callum Hudson-Odoi, 18


Bayern Munich wametupilia mbali mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Chelsea Callum Hudson-Odoi, 18, baada ya kutangaza kuwa hawatawasaini wachezaji wengine zaidi msimu huu. (Goal)

Eddie Nketiah atasalia katika uwanja wa Emirates baada ya uhamisho wake kuenda Augsburg kwa mkopo kugonga mwamba.

Mazungumzo kati ya Schalke na Tottenham kumhusu mshambuliaji wa Uholanzi Vincent Janssen, 24 yamegonga mwamba. (Football.London)

Udinese wameachana na azma yao ya kutaka kumsajili kiungo wa kati wa Derby,Tom Huddlestone, 32. (Derby Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Februari 1, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Ijumaa Februari 1, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/01/2019 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.