Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Februari 2, 2019


Manchester United watampa Ole Gunnar Solskjaer mkataba wa kudumu kama atafanikiwa kuifunga PSG kwenye Ligi ya Mabingwa.

Bayern Munich watarejea sokoni kusaka saini ya winga wa klabu ya Chelsea Callum Hudson-Odoi kwenye majira ya joto. 
(Sun)

Meneja wa klabu ya Newcastle Rafael Benitez yuko tayari kufanya mazungumzo ya mkataba mpya kufuatia usajili wa Miguel Almiron na Antonio Barreca.

Liverpool wanahofia Joe Gomez anaweza akahitaji kufanyiwa upasuaji kufuatia mguu wake ulioumia kushindwa kupona kwa wakati.

Xavi ameambia achukue kibarua cha mkurugenzi msaidizi wa kandanda katika klabu ya Barcelona ili 'asimamie mwisho wa Lionel Messi'.

Meneja wa klabu ya Tottenham Mauricio Pochettino amevunjwa moyo na kitendo cha klabu yake kushindwa kufanya usajili unaoeleweka katika madirisha mawili mfululizo. (Mirror)

West Ham wanahofia kuwa huenda Jack Wilshere akashindwa kurejea dimbani tena msimu huu kwa sababu ya majeraha yake kwenye kifundo cha mguu.

Hatimaye Tottenham wanatarajiwa kutaja tarehe ya uzinduzi wa uwanja wao mpya wenye thamani ya pauni bilioni 1 wiki ijayo.

Meneja wa klabu ya Arsenal, Unai Emery amemtaja meneja wa Manchester City Pep Guardiola kuwa ndiye kocha bora duniani. (Daily Mail)

Rafael Benitez amedai kuwa hakutishia kuondoka Newcastle baada ya klabu yake kusajili wachezaji wawili siku ya kufungwa kwa dirisha la usajili.

Ivan Perisic 

Meneja wa Inter Milan, Luciano Spalletti anaamini Arsenal ilionyesha "dharau" kwa winga Ivan Perisic kwa kupendekeza uhamisho wake kwenye dirisha la usajili mwezi Januari. (Independent)

Winga wa Chelsea Callum Hudson-Odoi hatasaini mkataba mpya Stamford Bridge baada ya kuzuiliwa kujiunga na Bayern Munich mwezi Januari. 
(Times)
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Februari 2, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Februari 2, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/02/2019 07:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.