Loading...

Watanzania wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi


Timu nyingi za Taifa barani Afrika hunufaika zaidi kutokana na wachezaji wao wanaochezea sehemu mbali mbali nje ya nchi, hii inaaminika kuwa huleta changamoto mpya na uzoefu ndani ya vikosi vyao pindi wanapo liwakilisha taifa katika michuano.

Taifa kama Algeria limekuwa likinufaika zaidi na mfumo huo wa kuwa na wachezaji wengi wanaochezea kwenye klabu za nje ya nchi ambao wamekuwa na uzoefu mkubwa katika soka la ushindani, miongoni mwa mataifa mengine yanayonufaika ni Ghana, Cameroon, Misri na Nigeria.

Wachezaji wa Tanzania siku za hivi karibuni wamekuwa wakipata soko kwenye nchi za nje huku idadi kubwa ikizidi kuongezeka.

Wachezaji wa Tanzania siku za hivi karibuni wamekuwa wakipata soko kwenye nchi za nje huku idadi kubwa ikizidi kuongezeka.

Mbwana Samatta

Miongoni mwa wachezaji wa Tanzania waliyopata nafasi ya kusajiliwa kwenye klabu za nje ya nchini ni pamoja na Mbwana Samatta.

Mbwana Samatta ni mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania aliyepata nafasi ya kuzichezea klabu ya Simba, TP Mazembe ya DR Congo kisha kutimkia KRC Genk ya nchini Ubelgiji.

Saimon Msuva

Saimon Msuva mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) na klabu ya Difaa El Jadida ambapo ametokea Dar es Salaam Young African.

Abdi Banda ni beki kisiki wa timu ya Taifa ya Tanzania ambaye anaichezea klabu ya Baroka FC ya nchini Afrika Kusini akitokea Simba SC.
Thomas Ulimwengu

Thomas Ulimwengu mshambuliaji wa JS Saoura ya nchini Algeria raia wa Tanzania, akitokea Al- Hilal Club.

Eliud Ambukile aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Mbeya City amejiunga ambaye kwa sasa amejiunga na Black Leopards FC ya Afrika Kusini.

Rashid Mandawa mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya BDF XI ya Botswana inayocheza ligi kuu ya nchi hiyo akitokea Mtibwa Sugar.

Hassan Kessy beki wa klabu ya Nkana FC ya nchini Zambia akitokea kwenye timu ya Yanga lakini pia akiwahi kuichezea Simba ya Tanzania.

Ally Hamisi Ng’anzi ni mchezaji wa klabu ya MFK VySkov ya daraja la pili barani Ulaya ambayo ipo Jamhuri ya Czech akitokea Singida United.

Adi Yussuph mshambuliaji wa Tanzania anayekipiga kwenye klabu ya Solihull Moors Football Club ya nchini Uingereza akitokea Barrow AFC ya hapo hapo England.

Himid Mao Mkami (Ninja) ni kiungo tegemezi wa timu ya taifa ya Tanzania ambaye kwa sasa anakipiga kwenye klabu ya Petrojet FC ya Misri akitokea Azam FC.

Yahya Zayd mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anakipiga kwenye klabu ya Ismaily SC ya nchini Misri akitokea Azam FC.

Shiza Ramadhan Kichuya winga mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania aliyekuwa anaichezea klabu ya Simba ambaye kwa sasa ni mchezaji halali wa Enppi SC inayoshiriki ligi kuu nchini Masri.

Shaaban Idd Chilunda ni nyota wa Tanzania anayekipiga klabu ya CD Izarra inyoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania akitokea Azam FC.

Farid Mussa mshambuliaji mwenye kasi na uwezo wa kutembea na mpira kwenye winga ya kushoto na kulia na kuwafanya vibaya mno mabeki wazembe anakipiga kwenye klabu ya Deportivo Tenerife ya Ligi Daraja la Pili Hispania akitokea Azam FC.

Majina hayo 14 ya wanasoka wanaokipiga nchi mbali mbali duniani ni wale wanaozungumzwa tu midomoni mwa wapenda mpira lakini wapo wengi ambao hawafahamiki ila wanasukuma gozi huko huhaibuni na wengine wakiwa katika majaribio kama beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Job akiwa FC Arsenal Kyiv, Ndemla na wengine.
Watanzania wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi Watanzania wanaosakata soka la kulipwa nje ya nchi Reviewed by Zero Degree on 2/02/2019 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.