Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Februari 16, 2019


Inadaiwa kuwa Mesut Ozil amekataa kuondoka Arsenal, licha ya Unai Emery kumwambia aondoke.

Muda wa Marcelo katika klabu ya Real Madrid uko ukingoni baada ya kocha Solari kuanza kuonyesha imani zaidi kwa wachezaji chipukizi. (talkSport)

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil, hataondoka klabu hiyo kwa mkopo msimu ujao katika jaribio la Gunners kubana matumizi.

Kuna tetesi kiungo huyo wa Ujerumani wa miaka 30 hana mpango wa kurejea klabu hiyo. (Daily Mail)

Beki wa kati wa Inter Milan na Slovakia Milan Skriniar, 24, ni miongoni mwa wachezaji wanaolengwa na Manchester United, wengine ni pamoja na mlinzi wa Napoli raia wa Senegal Kalidou Koulibaly, 27, na Joachim Andersen, 22 wa Sampdoria. (Independent)

Chelsea wanaamini kuwa wanaweza kumsajili moja kwa moja mshambuliaji raia wa Argentina Gonzalo Higuain, 31, kwa chini ya euro milioni 36 kama walivyokubaliana na Juventus hapo awali. (ESPN)

Mlinzi wa Chelsea Gary Cahill, 33, ameshangazwa na hatua ya kuachwa kwake nje ya kikosi kitakacho kabiliana na Malmo katika mchuano wa ligi ya Europa baada ya 'The Blues' kupewa kipigo cha mabao 6-0 na Manchester City Jumapili iliyopita. (Telegraph)

Mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente, 33, amesema"atafurahia sana" kusalia Tottenham kwa mwaka mmoja zaidi. (Evening Standard)
Manchester United wanapania kumnunua winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho, 18, ambaye thamani yake inakadiriwa kuwa euro milioni 70 baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kumnunua kutoka Manchester City kwa euro milioni nane mwaka 2017.

Arsenal wanataka kumsajili mkurugenzi wa soka haraka iwezekanavyo na wanaopigiwa upatu kuchukua nafasi hiyo ni Marc Overmars wa Ajax ama Monchi kutoka Roma.

Kipa wa Manchester United Sergio Romero, 31, anayeng'ang'aniwa na vilabu kadhaa za Ulaya ikiwa ni pamoja na Boca Juniors, lakini raia huyo wa Argentina hana mpango wa kuhama Old Trafford. (Sun)

Msambuliaji wa klabu ya Benfica Joao Felix,19

Barcelona na Real Madrid wamewatangulia Manchester United katika juhudi za kumsaini mshambuliaji hatari wa Benfica Joao Felix,19, raia wa Ureno.

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema mshambuliaji wa France Nabil Fekir,25 ambaye analengwa na Liverpool na Chelsea, anakaribia kusaini makubaliano ya kurefusha mkataba wake katika klabu hiyo ya Ufaransa. (Mirror)

Meneja wa Manchester City Pep Guardiola amesema ''anasikitika'' kuwa hakuweza kumsaini aliyekuwa nyota wa Leicester City Riyad Mahrez, 27, kwa pauni milioni 60. (Manchester Evening News)

Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Februari 16, 2019 Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumamosi Februari 16, 2019 Reviewed by Zero Degree on 2/16/2019 08:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.