Vikosi vinavyotarajiwa kuanza leo Yanga Vs Simba
- Soma zaidi: Simba SC yapata kocha msaidizi
Yanga ambayo inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 58, itakuwa mwenyeji wa mchezo huo utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga ambacho kimepiga kambi mkoani hapa tangu Jumatatu ya wiki hii, kimekuwa kikifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Chuo cha Biblia uliopo Bigwa.
- Soma zaidi: Kuelekea mechi ya watani, Yanga yapigwa faini
Katika mazoezi ya jana asubuhi, Zahera raia wa DR Congo, alionekana kuwa makini na kikosi ambacho kinaaminika ndicho kitaanza katika mchezo huo wa kesho.
Kikosi hicho kilikuwa kinaundwa na Ramadhan Kabwili, Paul Godfrey ‘Boxer’, Gadiel Michael, Andrew Vincent ‘Dante’, Kelvin Yondani, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Mrisho Ngassa, Feisal Salum ‘Fei Toto’, Heritier Makambo, Papy Tshishimbi na Ibrahim Ajibu.
Aussems kushangaza wengi:
Aussems kushangaza wengi:
KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, leo Jumamosi anaweza kuwashangaza wengi kwa namna ambavyo atapanga kikosi chake cha kwanza kuna uwezekano mshambuliaji tegemeo timu hiyo, Emmanuel Okwi, akaanzia benchi.
Licha ya Aussems kusema kutakuwa na mabadiliko kwenye kikosi chake cha leo, lakini kuna uwezekano mkubwa wa kikosi hicho kikawa hivi; Aishi Manula, Zana Coulibaly, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Juuko Murshid, Pascal Wawa, James Kotei, Clatous Chama, Jonas Mkude, John Bocco, Meddie Kagere na Hassan Dilunga.
Vikosi vinavyotarajiwa kuanza leo Yanga Vs Simba
Reviewed by Zero Degree
on
2/16/2019 08:40:00 AM
Rating: