Unai Emery ashindwa kujizuia kwa Iwobi
Unai Emery amesifu kuwango cha Iwobi lakini ameweka wazi tamaa yake ya kuona nyota huyo akifanya mambo makubwa zaidi.
Kulingana na OneFootbal, meneja huyo wa Arsenal alivutiwa na kiwango cha Alex Iwob dhidi ya Huddersfield Town walipoibuka na ushindi wa mabao 2-1 siku ya Jumamosi, lakini anafikiri kuwa winga huyo raia wa Nigeria ana nafasi kubwa ya kufanya vizuri zaidi.
Iwobi aliifungia Arsenal bao la kuongoza katika dimba la John Smith, wakati alipo jaribu kupiga mpirra golini uliomgusa beki na kuingia wavuni. Lilikuwa ni goli lake la tatu msimu huu, akilinganisha na idadi ya mwaka uliopita, licha ya kuanza na kikosi cha kwanza katika michezo michache.
Mnigeria huyo mwenye umri wa miaka 22 alifanya makubwa mwanzoni mwa msimu na ilionekana kama atakuwa kiungo muhimu menejimenti mpya. Lakini kiwango chake kilionekana kushuka katika wika chache zilizopita.
Emery anaamini nyota huyo ana mtazamo mzuri na anataka afanye maboresho katika maeneo kadhaa. Mreno huyo alisema: “Bado ana umri mdogo, anajitoa kwa moyo na ana mwili uliojengeka vizuri.
“Anahitaji kuboresha mbinu zake, labda, lakini zaidi ya yote ni mtulivu akiwa na mpira kutafuta uaidizi rahisi zaidi katika lango la adui, kutafuta uwezekano wa kufunga, au kutafuta chaguzo zuri zaidi, kama ni kupiga mpira au kukokota.
“Alifunga goli [Jumamosi], alipata nafasi nyingine nzuri iliyokalibia kuwa 'assist' kwa Lacazette, lakini nafikiri mechi yake ya kwanza – kuanza na kikosi cha kwanza na mtazamo wake – ulikuwa mkubwa sana, na kiwango chake kilikuwa kizuri sana.”
Arsenal itacheza na BATE Borisov Alhamisi hii kwenye Europa League, ikiwa ni mchezo wao wa kwanza wa hatua ya 32 bora. Haitakuwa rahisi kwa washika bunduki hao kwenye mbio hizo za kuwania taji msimu huu.
Unai Emery ashindwa kujizuia kwa Iwobi
Reviewed by Zero Degree
on
2/11/2019 09:05:00 AM
Rating: