Loading...

Boeing kulipa fidia kwa familia za wafiwa


Kampuni ya ndege ya Boeing imetangaza kulipa TZS 332 milioni kwa kila familia iliyopoteza ndugu katika ajali za ndege za Ethiopia na Indonesia zilizohusisha ndege aina ya Boeing 737 Max.

Baadhi ya mawakili wanaotetea familia hizo wamesema fidia hiyo haitakuwa na msaada, kwani ndugu wa wahanga wanataka majibu kamili kuhusu ajali hiyo.

Ikumbukwe kuwa ajali hiyo ilitokea mwezi Machi mwaka huu, ambapo ilikuwa ikisafiri kutoka mjini Adis Ababa kuelekea Nairobi, taarifa za kampuni ya ndege ya Ethiopia Airlines zilisema kulikuwa na abiria kutoka nchi 33 waliokuwa wakisafiri na jumla ya watu 157 walipoteza maisha.

Familia ziliombwa kutoa sampuli ya vinasaba kwa Lengo la kupata utambuzi wa miili ya ndugu zao, na katika kipindi hicho nchi mbalimbali duniani zilizuia matumizi ya ndege aina Boeing 737, baada ya wengi kufananisha tukio hilo na lile la Lion Air Flight 610 lililotokea mwaka 2018 ambapo ndege ya Boeing 737 Max 8 ilidondoka muda mfupi baada ya kupaa.
Boeing kulipa fidia kwa familia za wafiwa Boeing kulipa fidia kwa familia za wafiwa Reviewed by Zero Degree on 9/25/2019 07:25:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.