Fatma Karume kujiunga na siasa
Hatua hiyo inajiri siku chache tu baada ya mahakama kumzuia kuendelea kutoa huduma za uwakili katika eneo la Tanzania bara kutokana na kesi iliofunguliwa na katibu wa uenezi wa chama cha ACT wazalendo Ado Shaibu akipinga uteuzi wa mwanasheria mkuu wa serikali Adelardus Kilangi.
Kwa mujibu wa taarifa ya BBC, Bi fatma alisema kwamba pengine hiyo ndio njia pekee iliyosalia kwa yeye kufanikiwa kuleta mabadiliko nchini.

Licha ya kwamba hakusema ni chama gani ambacho huenda akakitumia katika safari yake mpya, Bi Fatma amesema kwamba siasa pekee ndio suluhisho la mabdiliko nchini.
''Siasa ndio inaleta mabadiliko, imeleta mabadiliko Kenya, imeleta katiba mpya'' sijajua ni chama gani lakini nafanya utafiti wa kuangalia kipi kitaendana na fikra zangu''
Amasema kwamba anasikitishwa na jinsi mahakama zinavyofanya kazi nchini na kusisitiza kuwa kuhamia kwake katika siasa kunaweza kuwa suluhu la haki kwa wananchi wa kawaida.
''Nilidhani kuwa mahakama ingeleta mabadiliko lakini sio kweli, siasa inaweza kuleta mabadiliko zaidi, kama mimi nafutwa kufanya kazi zangu jambo ambalo ni haki yangu ya msingi, watu wa kawaida watakua wanapatwa na mambo makubwa zaidi''
Fatma ni mwanasheria mkongwe na mtoto wa aliyekua rais wa awamu ya tano wa Zanzibar Amani Karume na mjukuu wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Abeid Karume.
Kwa kipindi kirefu amekuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali ya Tanzania.
Anasema kuwa jina la familia yake halijasababisha yeye asikumbwe na vikwazo anavyokutana navyo.
''jina la familia yangu halina uhusiano wowote na namna ninavyoishi nchi hii, jengo hili la ofisi lilipuliwa lakini polisi hawakufanya uchunguzi wowote na jina langu halikuchangia''

Baada ya kusimamishwa kwake kuhudumu kama wakili katika eneo la Tanzania bara haijulikani ni lini hasa ataweza kuendelea kushiriki katika mahakama za Tanzania bara, hadi pale kamati ya mawakili Itakavyokaa na kuamua hatma yake.
Hatahivyo Fatuma Karume amesema kuwa maamuzi hayo yametolewa bila yeye kusikilizwa.
Kwa upande wa yeye kuendelea na shughuli zake, amesema kuwa atafungua kesi za kikatiba upande wa Zanzibar.
''Nina mpango wa kufungua kesi Zanzibar, kuna hii ya Uamsho, wapo ndani miaka sita sasa na kesi haijulikani ikoje, nitaifungua upya na kesi zingine za kikatiba''

Mnamo mwezi Agosti mwaka 2017 makao makuu ya kampuni ya mawakili inayomilikiwa na wakili Bi Fatma Karume yalikumbwa na mlipuko wa bomu.
Kampuni hiyo inaorodhesha kampuni za mawasiliano, kawi, benki pamoja na serikali kama mojawapo ya wateja wake.
Wakati huo bi Karume alikuwa akimwakilisha aliyekuwa kiranja wa upinzani bungeni Tundu Lissu mahakamani kwa mashtaka ya kuitusi serikali.
Wakaazi wa eneo hilo katikati mwa mji wa Dar es Salaam wanasema walisikia misururu ya milipuko mikubwa kabla ya jumba hilo kujaa moshi na vifusi.
Mashahidi walisema kuwa walipata kifaa cha bomu la bomba.
Mmoja wa mawakili wa kampuni hiyo alisema kuwa afisi yao iliharibiwa lakini hakuna kilichoibwa.

Reviewed by Zero Degree
on
9/25/2019 07:20:00 AM
Rating: