Mtoto wa Mkuu wa Majeshi Tanzania afariki dunia kwa ajali ya ndege
Nelson alikuwa rubani wa ndege hiyo iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania. Ndege hiyo ilianguka saa 1:30 asubuhi wakati ikipaa katika uwanja huo kwenda mkoani Arusha.
Habari za uhakika kutoka mamlaka ya viwanja wa ndege imeeleza kuwa Nelson aliondoka na ndege hiyo jana katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.
Akizungumza na Mwananchi katika uwanja wa ndege wa Soronera, msimamizi wa kampuni ya Auric, Peter Kimaro, amesema Nelson amefariki katika ajali hiyo akiwa na Nelson Orutu ambaye ni rubani mwanafunzi.
“Baada ya kuhakiki na kuona ndege iko sawa na kuruhusiwa kuruka kwenda Gurumeti kuwachukua wageni kuwapeleka KIA (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro), walipoingia na kuondoka na mimi nikajua wako sawa,” amesema na kubainisha kuwa Nelson ni mtoto wa mkuu huyo wa majeshi.
Amesema baada ya kuona ndege imeshika mwendo kisha ikapaa kidogo, badala ya kunyooka juu ikakata kona “na mimi nikashangaa kuona vile kisha ikagonga choo cha uwanjani na kuanguka na wote walifia ndani ya ndege.”
Amesema jeshi la zimamoto na uokoaji waliwahi kuzima moto na miili imehifadhiwa katika zahanati ya Soronera ikisubiri utaratibu mwingine.
Mtoto wa Mkuu wa Majeshi Tanzania afariki dunia kwa ajali ya ndege
Reviewed by Zero Degree
on
9/23/2019 05:05:00 PM
Rating: