Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Septemba 24, 2019
Meneja wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer, mwenye umri wa miaka 46, ni mtu wa pili miongoni mwa watu wanaoweza kufukuzwa katika Primia Ligi - baada ya meneja wa Everton Mreno Marco Silva.
Mshambuliaji wa timu ya Ujerumani ya Bayer Leverkusen Kai Havertz, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia katika timu za Manchester United, Arsenal na Chelsea, amethamanishwa kwa kiwango cha pauni 90 . Kijana huyo mwenye umri wa miaka 20-alishinda magoli 17 katika michezo 34 ya Ligi ya Ujerumani - Bundesliga. (Sun)
Real Madrid wanafuatilia kwa karibu hali ya baadae ya uhamisho wa mchezaji wa safu ya mashambulizi wa Manchester City na England Raheem Sterling,mwenye umri wa miaka 24, ambaye alifunga magoli saba katika michezo minane kwa klabu na nchi yake msimu huu. (El Mundo Deportivo)
Manchester United wameanzisha mazungumzo na kiungo wa kati Paul Pogba kuhusu mkataba mpya. Pogba mwenye umri wa miaka 26 ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa amebakiza miaka miliwi katika mkataba wake wa sasa. (Times)
Liverpool wanakaribia kukamilisha mkataba wa mavazi ya kimichezo na watengenezaji wa jezi Nike kuanzia msimu ujao. (Telegraph)
Manchester United wanatarajiwa kutangaza rekodi ya mapato yao ya mwaka ambayo yatakuwa makubwa kwa kiwango cha pauni milioni 615 zaidi Jumanne.
Barcelona wanaangalia uwezekano wa kusaini mkataba na winga wa Reign FC Megan Rapinoe mwenye umri wa miaka 34. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Marekani alishinda tuzo ya mwanasoka bora mwanamke katika Tuzo ya mchezaji bora wa FIFA mjini Milan Jumatatu. (ESPN)
Aston Villa na West Brom wanamtaka kiungo wa safu ya nyuma -kushoto ya England Muingereza Sam McCallum mwenye umri wa miaka 19.
West Ham imewezesha kusitisha mipango ya kupata haki ya mkataba wa kuupatia jina uwanja wa London Shadi kufikia mwisho wa msimu. (Football Insider)
Mshambuliaji wa Chelsea Mbrazil Willian anafuatiliwa kwa karibu na timu ya Juventus, ambao wanaweza kumchukua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31- wakati mkataba wake utakapomalizika msimu ujao . (Sky Sports)
Mchezaji wa safu ya mashambulizi ya Juventus Mcroatia Mario Mandzukic, mweney umri wa maika 33, ana matumaini ya kupata nafasi katika Primia Ligi mwezi Januari. (Tuttosport)
Chelsea wanayo matumaini ya kumuajiri kiungo wa mashambulizi wa kikosi cha England cha vijana wenye chini ya umri wa miaka 21 Fikayo Tomori, mwenye umri wa miaka 21, na inatumainiwa kuwa atasaini mkataba wa miaka mitano katika wiki chache zijazo. (La Gazzetta dello Sport)
Fikayo Tomori, 21 |
AC Milan wanamlenga mlinzi wa Tottenham mwenye umri wa miaka kutoka Ivory Coast Serge Aurier kwa uhamisho. (Sport Mediaset)
Mshabiki wa Chelsea wanasema kuwa kuondolewa kwa bango la Eden Hazard kabla ya gemu dhidi ya Liverpool lilikuwa ni kosa kwani klabu hiyo iliwapatia mashabiki mabango yasiyofaa kujonyesha. (Standard)
Peterborough United wamewapatia ofa watumishi wa kampuni ya ndege ya Thomas Cook tiketi za bure za kutazama mchezo wa Jumamosi dhidi ya AFC Wimbledon kufuatia kufilisika kwa kampuni hiyo ya safari ambayo ina makao makuu katika mji huo. (Mail)
Peterborough United wamewapatia ofa watumishi wa kampuni ya ndege ya Thomas Cook tiketi za bure za kutazama mchezo wa Jumamosi dhidi ya AFC Wimbledon kufuatia kufilisika kwa kampuni hiyo ya safari ambayo ina makao makuu katika mji huo. (Mail)
Chanzo: BBC
Tetesi za soka barani Ulaya leo Jumanne Septemba 24, 2019
Reviewed by Zero Degree
on
9/24/2019 07:20:00 AM
Rating: