Loading...

11 wafariki dunia kwenye mlipuko Morogoro


Watu 11 wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa katika mlipuko uliotokea katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha Mtibwa kilichopo wilayani Mvomero, mashariki mwa Tanzania.

Tukio hilo linaloendelea kuchunguzwa limetokea katika wilaya hiyo iliyopo mkoani Morogoro, takriban kilomita 370 (maili 230) magharibi mwa jiji kuu la kibiashara la Dar es Salaam.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa polisi wa mkoa wa Morogoro, Alex Mkama amesema mlipuko huo ulitokea jana usiku na timu ya wataalamu kutoka jeshi la uokozi linaendelea kuchunguza chanzo.

“Bado hatujapata chanzo halisi cha mlipuko huo, lakini timu zetu ziko hapa tangu juzi usiku kufanya uchunguzi,” alisema Kamishna Mkama huku zikiwepo taarifa kuwa kiwanda hicho kimesitisha uzalishaji wa sukari baada ya bomba la kusafirishia mvuke kupasuka.

Taarifa zaidi zinaeleza kuwa miongoni mwa waliofariki ni raia wa Tanzania, Brazil, India, China na Kenya.

Mwaka 2019, zaidi ya watu 100 walipoteza maisha na makumi kadhaa kujeruhiwa baada ya lori la mafuta kulipuka katika mji wa Morogoro.
11 wafariki dunia kwenye mlipuko Morogoro 11 wafariki dunia kwenye mlipuko Morogoro Reviewed by Zero Degree on 5/23/2024 06:54:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.