Loading...

Baba apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wake


Mkazi wa Nyakato mkoani Mwanza, Bashir Mohamed (35) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya Ilemela kwa kosa la kufanya mapenzi na mtoto wake (jina limehifadhiwa).

Mohamed alipandishwa mahakamani hapo juzi na kusomewa shtaka katika kesi ya jinai namba 13448/2024 ambapo anadaiwa kulitenda kati ya Septemba mwaka jana hadi Februari 15 mwaka huu.

Akisoma shtaka hilo, Mwendesha Mashtaka wa serikali, Mwanahawa Changale, alisema mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kwa nyakati tofauti kati ya Septemba, 2023 hadi Februari.

Aidha, alisema mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na Kifungu Namba 158 (1) (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Jinai Aya ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2022.

Baada ya kusomewa shtaka hilo, mshtakiwa alikana na kuomba kupewa dhamana akisema shtaka linalomkabili linadhaminika.

Baada ya maelezo hayo, Hakimu Mkazi Mwandamizi, Juma Opudo alimtaka mshtakiwa kuitimiza masharti ya dhamana ambayo ni kuwa na wadhamini wawili watakosaini hundi ya maneno ya Sh.milioni nne kila mmoja na mwingine awe na mali isiyohamishika.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo kwani barua ya udhamini ya mdhamini mmoja aliyetokea wilayani Magu haikuthibitishwa na Hakimu Mfawidhi wa wilaya yake.

Hakimu Opudo aliahirisha shauri hilo hadi Juni 11, mwaka huu litakapoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kuanza kusomewa hoja za awali.
Baba apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wake Baba apandishwa kizimbani kwa tuhuma za kufanya mapenzi na mtoto wake Reviewed by Zero Degree on 5/23/2024 05:17:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.