Loading...

Rais wa Iran Ebrahim Raisi afariki dunia katika ajali ya helikopta


Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian na wengine kadhaa wamethibitishwa kufariki dunia katika ajali ya helikopta iliyotokea Jumapili kaskazini-magharibi mwa Iran, televisheni ya taifa imesema.

Majina ya baadhi ya waliofariki katika ajali hiyo ya helikopta kando na Rais wa Iran Ebrahim Raisi na Waziri wa Mambo ya Nje Hossein Amir-Abdollahian sasa yametolewa.

Shirika la habari la serikali IRNAA linasema kwamba ndani ya ndege hiyo pia alikuwemo Ayatollah Mohammad Ali Al-e Hashem, imamu wa Swala ya Ijumaa katika mji wa Tabriz, na Jenerali Malek Rahmati, gavana wa jimbo la Irani la Azabajani Mashariki.

Kamanda wa kitengo cha ulinzi wa rais, Sardar Seyed Mehdi Mousavi, pia aliuawa, pamoja na walinzi kadhaa na wafanyakazi wa helikopta ambao bado hawajatajwa.

BBC
Rais wa Iran Ebrahim Raisi afariki dunia katika ajali ya helikopta Rais wa Iran Ebrahim Raisi afariki dunia katika ajali ya helikopta Reviewed by Zero Degree on 5/20/2024 10:28:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.