Loading...

Wakazi wa Nairobi watakiwa kuwa waangalifu dhidi ya simba wanaozurura mitaani


Mamlaka ya wanyamapori nchini Kenya imewataka wakazi wa eneo la Lang'ata jijini Nairobi kuwa waangalifu kufuatia ripoti za simba watatu wanaodaiwa kuonekana karibu na eneo hilo.

Siku ya Alhamisi, maafisa wa Shirika la Huduma ya Wanyamapori (KWS) walitumwa kuwatafuta simba hao walioripotiwa kuonekana karibu na Gereza la Wanawake la Langata viungani mwa jiji.

Lakini simba hao hawakupatikana baada ya msako mrefu wa usiku, KWS ilisema kwenye taarifa.

Hata hivyo, ilisema maafisa bado wanafuatilia hali hiyo kwa karibu na wako katika hali ya tahadhari "kuhakikisha usalama wa umma unapewa kipaumbele," iliongeza.

Wakazi walihimizwa kuripoti tukio lolote la wanyamapori katika eneo hilo.

Hii sio mara ya kwanza simba wanaripotiwa kutoroka kutoka mbuga ya wanyama ya Nairobi, ambayo inasifiwa kwa kuwa mbuga pekee duniani ndani ya jiji.
Wakazi wa Nairobi watakiwa kuwa waangalifu dhidi ya simba wanaozurura mitaani Wakazi wa Nairobi watakiwa kuwa waangalifu dhidi ya simba wanaozurura mitaani Reviewed by Zero Degree on 5/18/2024 07:03:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.