Baraza laingilia kati kupanda bei vocha
Sakata la kupanda kwa bei ya vocha za kukwangua limeifikia Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma za Mawasiliano (TCRA-CCC), ambalo limewaagiza watoa huduma za mitandao kuwadhibiti mawakala wanaopandisha bei bila kufuata utaratibu.
Aidha, limewashauri kutoa taarifa kwa watumiaji kutonunua vocha hizo na kuweka utaratibu wa kutoa malalamiko wanapokutana na kadhia hiyo ili kukomesha tabia hiyo mapema.
Hali hiyo imekuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu bei ya bidhaa hiyo kupanda kutoka Sh. 500 hadi 600 na Sh. 1,000 ikiuzwa hadi Sh. 1,200 huku kwenye karatasi zikiwa zimeandikwa bei ya awali.
Taarifa kwa umma iliyotolewa na baraza hilo hivi karibuni ilieleza kuwa kumekuwa na malalamiko ya watumiaji wa huduma za mawasiliano kuhusu kupanda kwa bei za vocha za simu za mkononi katika maeneo mbalimbali zikitofautiana baina ya wauzaji.
Kupitia taarifa hiyo, Katibu Mtendaji wa Baraza, Mary Msuya, alisema Baraza hilo lilipokea taarifa kupitia kamati za watumiaji za mikoa zikionyesha kuwa vocha ya Sh. 500 inauzwa kati ya Sh.550 hadi 600, Sh. 1,000 kuuzwa kati ya Sh. 1,100, hadi 1,200 kinyume na bei elekezi inayoonyeshwa kwenye vocha husika.
Alitaja mikoa ambayo Baraza limepokea malalamiko hayo kuwa ni Dar es Salaam, Rukwa, Iringa, Ruvuma, Manyara, Lindi, Mbeya, Mtwara na Songwe na linaendelea kufuatilia katika mikoa mingine kwa lengo la kupata taarifa zaidi ya bei hizo.
“Katika kushughulikia changamoto hiyo, Baraza limeshauriana na watoa huduma za mawasiliano ya simu kufuatilia mawakala wao na kupiga marufuku upandishaji holela wa bei za vocha,” alisema Mary.
Baraza limeshauri watumiaji wa huduma za mawasiliano kununua vocha kwa kupitia simu zao za mkononi wakati changamoto hii ikitafutiwa ufumbuzi na kuendelea kutoa taarifa za kupanda bei kiholela katika maeneo mbalimbali ya nchi ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria.
MADUKA MTAANI
Huko mitaani bado baadhi ya maduka yanauza vocha za kukwangua kwa bei ya Sh. 1,100 hadi 1,200 na mengine yakilazimika kutouza hali inayowaweka watumiaji katika wakati mgumu.
Leonard Urassa ni mmoja wa wanaouza vocha ya Sh.1,000 kwa Sh. 1,100 akitoa sababu kuwa analazimika kuuza hivyo ili kupata faida yake ya awali kwa kuwa ameuziwa na wakala wa jumla Sh. 980 kutoka Sh. 950 iliyokuwapo mwanzo.
Alisema pia anauza vocha ya Sh. 500 kwa Sh. 550 kwa sababu na ameinunua Sh. 480 kutoka Sh. 430 huku akikiri kuwa hatonunua tena vocha za aina hiyo kwa sababu hata upatikanaji wa wateja kwa sasa umekuwa mgumu wengi kuhamia kwenye vocha za kurusha.
Naye Athnat John anasema tangu mawakala wapandishe bei za vocha hizo ameacha kuzinunua kwa kuepuka hasara.
Changamoto hiyo pia iliibuliwa bungeni Mei 29, mwaka huu na Mbunge wa Viti Maalum, Tunza Malapo, aliyehoji serikali ina mpango gani juu ya kupanda kwa bei za vocha za kukwangua.
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Maryprisca Mahundi alisema wizara imewaagiza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kufuatilia suala hilo ili kuhakikisha kuwa watoa huduma za simu hawapandishi bei bila kufuata utaratibu.

Chanzo: Nipashe
Baraza laingilia kati kupanda bei vocha
Reviewed by Zero Degree
on
6/12/2024 03:40:00 PM
Rating: