Hali ya Mbappe si shwari
Kocha wa Ufaransa Didier Deschamps amesema nahodha Kylian Mbappe "hayuko vizuri" baada ya kupata jeraha baya la pua katika ushindi wao wa 1-0 dhidi ya Austria Jumatatu.
Wakati Philippe Diallo, rais wa Shirikisho la Soka la Ufaransa, aliwaambia waandishi wa habari mjini Duesseldorf kwamba Mbappe "hahitaji kufanyiwa upasuaji", kiwango cha jeraha lake bado hakijajulikana.
Mwishoni mwa mchezo wa ufunguzi wa Euro 2024 wa Ufaransa mjini Düsseldorf, Mbappe alipiga mpira kwa kichwa na uso wake ukagonga bega la Kevin Danso katika pasi ya kufuatisha.
Fowadi huyo mwenye umri wa miaka 25 alipokea matibabu uwanjani, akiwa na damu nyingi usoni, na kisha akatoka nje ya uwanja huku Ufaransa ikitaka kumtoa ili nafasi yake kuchukuliwa na Olivier Giroud.
Mchezo ulipoanza tena, Mbappe alienda uwanjani bila ruhusa na kuketi - hatua iliyomfanya kupewa kadi ya njano.
Nafasi yake ikachukuliwa na Giroud.
"Haendelei vizuri," kocha mkuu Didier Deschamps alisema katika mkutano na waandishi wa habari baada ya mechi.
Hali ya Mbappe si shwari
Reviewed by Zero Degree
on
6/18/2024 06:20:00 AM
Rating: