Loading...

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yawapiga msasa Wanasheria wa Serikali

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi waUmma na Utawala Bora, Mhe George Simbachaweneakizungumza na Mawakili wakati wa ufunguzi wa Mafunzomaalamu kwa Mawakili wa Serikali yaliyoandaliwa na Ofisi yaMwanasheria Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma hivi karibuni.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iliratibu na kuendeshamafunzo kwa Mawakili wa Serikali.

Mafunzo hayo yalilenga kuwajengea uwezo Mawakili kwenyemasuala mbalimbali yanayohusu sheria ikiwemo Uandishi washeria, mambo muhimu ya kuzingatia kwenye Mikataba naMakubaliano baina ya Nchi au Taasisi, pamoja na mambo yakuzingatia katika kuishauri Serikali kwenye nyanja ya Sheria.

Mafunzo hayo yalifanyika Jijini Dodoma hivi karibuni nakuhudhuriwa na Mawakili takribani mia mbili na tisini (290) kutoka taasisi mbalimbali za Serikali.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Jaji Dkt. Eliezer MbukiFeleshi akizungumza wakati wa mafunzo kwa Mawakili waSerikali yaliyoandaliwa na kuratibiwa na Ofisi hiyo JijiniDodoma.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe Jaji Dkt. Eliezer MbukiFeleshi akigawa vyeti kwa Mawakili kutoka Taasisi za Serikaliwalioshiriki mafunzo kwa Mawakili yaliyofanyika Jijini Dodoma.
Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yawapiga msasa Wanasheria wa Serikali Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali yawapiga msasa Wanasheria wa Serikali Reviewed by Zero Degree on 6/12/2024 04:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.