Loading...

Papa Francis aomba pande zinazozozana katika maeneo yenye migogoro kusitisha mapigano

Kiongozi wa Kanisa la Katoliki Papa Francis

Kiongozi wa Kanisa la Katoliki Papa Francis ameomba amani mashariki ya kati na sehemu nyingine duniani, na kutoa wito kwa pande zote zinazohusika katika mapigano kutoeneza vita hivyo.

Francis amesema kwamba anaendelea kufuatilia hali ilivyo mashariki ya kati kwa masikitiko makubwa.

Ameomba vita kusitishwa katika kila sehemu kuanzia Gaza, ambako hali ya kibinadamu ni mbaya sana.

Maelfu ya watu wameuawa au kujeruhiwa, na mamilioni ya raia wamekoseshwa makazi nchini Ukraine tangu Russia ilipoivamia na kuikalia kimabavu Crimea mwaka 2014, na kufuatiwa na vita Donbas na baadaye kuivamia Ukraine mwaka 2022.

Nchini Sudan, mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kati ya wanajeshi wa serikali na kikosi cha kijeshi cha dharura, yamekuwa yakiendelea tangu Aprili 2023, ambapo kati ya watu 13,000 na 15,000 wameuawa na zaidi ya 33,000 kujeruhiwa.

Watu milioni 7.7 wameachwa bila makazi na zaidi ya milioni 2 kukimbilia nchi nyingine.

Papa Francis amesema “aendelea kufuatilia hali katika mashariki ya kati kwa masikitiko makubwa. Nasisitiza ombi langu kwa pande zote husika kutoeneza na badala yake kusitisha vita mara moja, kuanzia Gaza ambako hali ya kibinadamu ni mbaya.”

“Naomba amani ya kweli ipatikane ili kumaliza mizozo. Naomba upendo uishinde chuki, na ulipizaji kisasi ugeuke kuwa msamaha,” aliongeza kiongozo huyo wa kanaisa la Katoliki.
Papa Francis aomba pande zinazozozana katika maeneo yenye migogoro kusitisha mapigano Papa Francis aomba pande zinazozozana katika maeneo yenye migogoro kusitisha mapigano Reviewed by Zero Degree on 8/08/2024 06:55:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.