Vilabu 24 bado havijafanya usajili - TFF
Zikiwa zimebaki siku saba tu kabla ya kufungwa kwa dirisha kubwa la usajili kwa madaraja mbalimbali nchini, jumla ya timu 24 bado hazijafanya usajili, zikiwamo tatu za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Taarifa iliyotolewa jana na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF), imesema kuwa hadi jana vilabu hivyo bado vilikuwa hazijaingiza majina ya wachezaji wake ambao itawatumia kwa msimu ujao wa mashindano.
Taarifa hiyo iliyosainiwa na Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF, Cliford Ndimbo, imezikumbusha klabu zote kuwa mwisho wa usajili ni Agosti 15, saa 5:59 usiku na hakutakuwa na muda wa ziada.
Imezitaja timu ambazo mpaka sasa bado hazijafanya usajili kwa timu za Ligi Kuu kuwa ni Tabora United, Fountain Gate na Dodoma Jiji.

Hata hivyo, TFF, imesema Tabora United na Fountain Gate zenyewe zimefungiwa kufanya usajili mpaka zitakapowalipa wachezaji wanaowadai.
Kwa upande wa timu za Ligi ya 'Championship' ambazo hazijakamilisha usajili wa wachezaji wake kwenye mfumo ni Biashara United, Mbeya Kwanza, TMA Stars, African Sports, Mtibwa Sugar, Gaita Gold, Stand United na Songea United.
Biashara United ina adhabu ya kufungiwa kusajili, hivyo nayo haiwezi kufanya hivyo mpaka itakapowalipa wachezaji wanaoidai timu hiyo.
Vilabu ambavyo havijafanya usajili mpaka sasa Ligi Daraja la Pili, maarufu kama 'First League' ni Tanesco, Nyumbu, Magnet, Tunduru Korosho, Dar City, African Lyon, Gunners FC, Hausing FC, Moro Kids, Pan African na Ruvu Shooting.

Zipo pia timu mbili za Ligi Kuu Wanawake ambazo hazijafanya usajili ambazo ni Ceasiaa Queens na Gets Program.
Vilabu 24 bado havijafanya usajili - TFF
Reviewed by Zero Degree
on
8/08/2024 10:05:00 AM
Rating: