Dk Magufuli balaa, vitanda 300 vyatua hospitali ya taifa Muhimbili.
Fedha za kununua vifaa tiba hivyo zilipatikana baada ya Rais John Magufuli kuamuru kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za kuwapongeza wabunge, zitumike kununua vifaa tiba katika hospitali hiyo.
Dar es Salaam. Wabunge wamepongeza kitendo cha kuwasilishwa Hospitali ya
Taifa ya Muhimbili (MNH) vitanda 300, magodoro 300, viti vya magurudumu 30,
blanketi 400 na mashuka 1,695 vilivyogharimu Sh251 milioni.
Fedha za kununua vifaa tiba hivyo zilipatikana baada ya Rais John Magufuli
kuamuru kiasi cha fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe za kuwapongeza
wabunge, zitumike kununua vifaa tiba katika hospitali hiyo.
Mbunge wa Mtambile (CUF), Masoud Abdallah Salum alisema uamuzi uliotolewa na
Rais upo sahihi kuekeleza fedha hizo zitumike kwa mahitaji ya huduma za
afya.
“Sina pingamizi kwa hilo kwa sababu ni jambo jema, lakini ni muhimu
kujihakikishia kama fedha hizo zimekwenda kufanya kazi husika pasipo kufanya
udanganyifu, maana kumekuwa na udhaifu sana wa matumizi sahihi ya fedha
zinakoelekezwa,” alisema.
Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba alisema kiongozi huyo ameanza
kuonyesha utekelezaji wa ahadi kwa vitendo. “Kama (Rais Magufuli) anavyosema
kwenye kaulimbiu yake ‘Hapa Kazi Tu’ ndiyo ameanza.
“Hata sisi (CCM) tunafurahi kwa sababu tumepata kiongozi ambaye Watanzania
walikuwa wanamtaka, kiongozi wa kuwatumikia wananchi wa kada zote na vyama vyote
bila kujali tofauti zao,” alisema.
Hata hivyo, Mbunge wa Chake Chake (CUF), Yussuf Kaiza Makame alisema Dk
Magufuli hakutakiwa kuzipangia matumizi fedha hizo, badala yake alipaswa
kulitumia Bunge liweke utaratibu wa kuzitumia.
Msemaji wa Bohari ya Dawa nchi (MSD), Ety Kusiluka alithibitisha bohari hiyo
kupeleka MNH vifaa tiba vya thamani ya Sh251 milioni ambavyo vilinunuliwa na
ofisi ya Bunge kwa agizo la Rais.
Alisema tayari vifaa hivyo vimepokelewa kwa ajili ya wagonjwa.
Credits: Mwananchi
Share this to all your friends.
Credits: Mwananchi
Share this to all your friends.
Dk Magufuli balaa, vitanda 300 vyatua hospitali ya taifa Muhimbili.
Reviewed by Zero Degree
on
11/23/2015 11:21:00 AM
Rating: