Ripoti ya EAC yaisifu Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Abdullah Mwinyi alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika kikao cha bunge hilo wakati akiwasilisha ripoti ya uchunguzi ya EAC.
Arusha.Tanzania imepunguza vizuizi vya barabarani na vituo vya ukaguzi kutoka 56 hadi sita ili kutekeleza Itifaki ya Soko la Pamoja la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Abdullah Mwinyi alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita katika kikao cha bunge hilo wakati akiwasilisha ripoti ya uchunguzi ya EAC.
Mwinyi alisema vizuizi na vituo vya ukaguzi vingi vilivyokuwa awali, vilichelewesha mizigo kufika kwa wakati na kuongeza gharama za kufanya biashara katika eneo la Afrika Mashariki.
“Kamati ilifanya kazi hiyo Novemba 8 hadi 12, 2015 kwa lengo la kuzifanyia utafiti changamoto za utendaji kwenye Ukanda wa Kati wa Usafirishaji kutoka Dar es Salaam hadi Rusumo mpaka wa Tanzania na Rwanda.
Mbunge wa EAC, kutoka Rwanda, Martin Ngoga alisema ripoti hiyo imeonyesha mwelekeo katika kutekeleza itifaki ya soko la pamoja. “Sina hakika wale watendaji wa Mamlaka ya Bandari (TPA) tuliokutana nao mwishoni mwa mwaka jana kama bado wapo, nasikia hapa Tanzania kila kitu ‘Hapa Kazi Tu’ wa,” alisema.
ZeroDegree.
Ripoti ya EAC yaisifu Tanzania.
Reviewed by Zero Degree
on
2/08/2016 10:01:00 PM
Rating: