YANGA kutoana jasho na TP MAZEMBE juani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
MCHEZO wa Kombe la Shirikisho kati ya Yanga dhidi ya TP Mazembe utapigwa Jumanne Juni 28 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, imeelezwa hivo.
Akizungumza jana, Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro alisema mchezo huo unatarajiwa kuwa wa ushindani baada ya Yanga kupoteza mchezo wao wa awali dhidi ya MO Bejaia ya Algeria.
Mkuu wa kitengo cha habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro.
“Mchezo wetu na TP Mazembe utaanza saa kumi kamili jioni na sisi Yanga tumejipanga kushinda ili kujihakikishia nafasi nzuri ya kuingia nusu fainali,” alisema Muro.
Awali, kulikuwa na uvumi kuwa timu hizo zitacheza usiku Jumatano ili kuwawezesha wengi kuushuhudia baada ya futari katika kipindi hiki cha mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Pia Muro alisema hali ya beki wa kushoto Oscar Joshua aliyeumia katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mo Bejaia anaendelea vizuri na atarejea uwanjani Jumanne na beki wa kulia Juma Abdul anaendelea vizuri kwani ameanza mazoezi mepesi mepesi.
Abdul alikosa mechi ya awali baada ya kuwa majeruhi kwa kuumia sehemu ya kifundo cha mguu na nafasi yake ilichukuliwa na Mbuyu Twite.
Yanga itawakosa Haji Mwinyi ambaye anatumikia adhabu ya kadi nyekundu na Amis Tambwe ambaye ana kadi mbili za njano. Kwa sasa Yanga inaendelea na mazoezi katika jiji la Antalya nchini Uturuki ikijifua kwani inahitaji matokeo mazuri ili kujiweka pazuri kwenye kundi lao.
ZeroDegree.
YANGA kutoana jasho na TP MAZEMBE juani kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Reviewed by Zero Degree
on
6/24/2016 10:48:00 AM
Rating: