Loading...

Mgombea urais wa chama cha Democrat, Hillary Clinton ashitakiwa.

JAJI wa Mahakama mjini Washington amesema mgombea urais wa chama cha Democrat, Hillary Clinton, lazima ajibu mashtaka yaliyowasilishwa na kundi la wahafidhina kuhusu matumizi mabaya ya barua pepe.


Kundi hilo la wakereketwa wasiopendelea mabadiliko, Judicial Watch, limeishtaki wizara ya mambo ya nje juu ya suala hilo likimtaka Clinton kutoa ushahidi binafsi chini ya kiapo kuhusu kilichotokea wakati akiongoza wizara hiyo.

Hatua hiyo inakuja baada ya Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) kukamilisha uchunguzi wake mwezi uliopita, bila kupendekeza mashtaka yoyote dhidi ya Clinton.

Wanasheria wa Judicial Watch, walitaka wamfanyie Clinton mahojiano chini ya kiapo kama sehemu ya kesi yao ya Sheria ya Uhuru wa Habari dhidi ya wizara hiyo.

Lakini pia Jaji Emmet Sullivan alisema kundi hilo limeshindwa kuonesha kuwa haliwezi kupata ukweli inaoutafuta kwa njia nyingine zenye changamoto kidogo.

Amelipa kundi hilo hadi Oktoba 14 kumpatia Clinton maswali huku naye akipewa siku 30 kuyajibu kimaandishi.

Iwapo kundi hilo linataka kumuuliza maswali ya ufuatiliaji kimaandishi, linatakiwa kwenda kwa jaji kupata kibali.

Kundi hilo linatafuta maelezo ya uhusiano wa Huma Abedin na wizara ya mambo ya nje, ambao uliruhusu kufanya kazi za nje wakati akiwa msaidizi mwandamizi wa Waziri Clinton.

Lakini msemaji wa timu ya kampeni ya Clinton, Brian Fallon alisema kesi hiyo, ni njama nyingine zinazolenga kuibomoa kampeni ya Hillary Clinton.

Credits: Mtanzania
ZeroDegree.
Mgombea urais wa chama cha Democrat, Hillary Clinton ashitakiwa. Mgombea urais wa chama cha Democrat, Hillary Clinton ashitakiwa. Reviewed by Zero Degree on 8/22/2016 08:30:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.