Loading...

Mkenya apokonywa medali ya Shaba mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Kemboi alitwaa dhahabu Michezo ya Olimpiki ya London 2012
Bingwa wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji kutoka Kenya Ezekiel Kemboi amenyang'anywa medali yake ya shaba aliyoishinda mjini Rio de Janeiro, Brazil.

Kemboi, 34, aliyemaliza wa tatu katika mbio hizo, alikuwa amepewa nishani ya shaba.

Lakini Ufaransa ilikata rufaa baada ya kubainika kwamba mwanariadha huyo wakati mmoja, baada ya kuruka kiunzi na maji, alikanyaga nje ya mstari wakati akishiriki mbio hizo Jumatano.

Mfaransa Mahiedine Mekhissi, aliyemaliza nafasi ya nne, amepandishwa hadi nafasi ya tatu na kupewa nishani ya shaba.

Kemboi, aliyeshinda Olimpiki za London 2012 katika michezo ambayo Mahiedine Mekhissi-Benabbad alishinda fedha, tayari ametangaza kwamba atastaafu.

Mshindi wa mbio hizo za Rio alikuwa Mkenya Conseslus Kipruto ambaye pia aliweka rekodi mpya ya Olimpiki , muda wake ukiwa 8:03.28.


Corneslus Kipruto
Mmarekani Evan Jager alimaliza wa pili muda wake ukiwa 8:04.28.

Muda wa Kemboi ulikuwa 8:08.47 na wa Mekhissi 8:11.52.

Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
Mkenya apokonywa medali ya Shaba mjini Rio de Janeiro, Brazil. Mkenya apokonywa medali ya Shaba mjini Rio de Janeiro, Brazil. Reviewed by Zero Degree on 8/18/2016 12:47:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.