Loading...

Trump amteua mkosoaji mkubwa wa biashara za China kuwa msimamizi wa bodi ya biashara.

Rais mteule wa Marekani Donald Trump, amemtaja mkosoaji mkubwa wa biashara za Kichina Peter Navarro kuwa kiongozi mkuu wa baraza jipya la kibiashara katika Ikulu ya White House.

Peter Navarro, alizindua sera ngumu dhidi ya Beijing na akaandika kitabu kwa jina "Death by China: How America Lost its Manufacturing Base". Yani kifo cha China: namna Marekani ilipopoteza uwezo wake wa uundaji bidhaa"

Serikali ya mpito ya Doland Trump, imemsifu kwa uwezo wake wa kufufua uchumi, mbali na kukabiliana na uhaba wa kazi kwa Wamarekani.

Peter Navarro mkoasoaji mkubwa wa Biashara za China.
Bwana Trump pia, ameteua mwekezaji bilionea na msomi wa uchumi, Carl Icahn, kama mshauri mkuu wa mageuzi.

Bw Icahn, amesema kuwa biashara nchini Marekani, imelemazwa na masharti mengi yasio na maana.

Credits: BBC Swahili
ZeroDegree.
Trump amteua mkosoaji mkubwa wa biashara za China kuwa msimamizi wa bodi ya biashara. Trump amteua mkosoaji mkubwa wa biashara za China kuwa msimamizi wa bodi ya biashara. Reviewed by Zero Degree on 12/22/2016 10:52:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.