Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akumbukwa akiwa gerezani.
Waziri Mkuu mstaafu Frederick Sumaye akiwasili kwenye Gereza la Kisongo, Arusha kumjulia hali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema jana. |
Mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye jana kwa nyakati tofauti walikwenda katika Gereza la Kisongo kumjulia hali, Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na kueleza kwamba wamemkuta akiwa imara huku wakiomba haki itendeke.
Lema yupo mahabusu, tangu Novemba 8 mwaka jana, baada ya dhamana yake kupingwa na Jamhuri, katika kesi za jinai namba 440/2016 na 441/2016 za kutoa lugha za uchochezi dhidi ya Rais John Magufuli.
Akizungumza na jana mara baada ya kupokea ujumbe wa viongozi hao ha zamani wa Serikali, Meya wa Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema Lowassa ndiye aliyekuwa wa kwanza kufika Arusha alimuongoza gerezani kuonana na Lema.
Alisema Lowassa alifika Magereza saa tano asubuhi na baada ya kukamilisha taratibu, alipata fursa ya kuzungumza na Lema kwa takriban saa 1:15.
Lazaro alisema miongoni mwa mambo ambayo, Lowassa alizungumza na Lema ni kumtaka kuwa imara na kwamba haki yake itapatikana.
Akiwa nje ya gereza hilo, Lowassa alisema anaamini Mahakama itatenda haki katika kesi ya Lema na akaiomba kutimiza wajibu wake.
Lowassa alisema Watanzania bado wana imani kubwa na Mahakama kwani ndicho chombo pekee ambacho kinapaswa kufanya kazi kikiwa huru.
Muda mfupi baadaye, Sumaye akiongozwa na Naibu Meya wa Jiji la Arusha, Viora Likindikoki alifika katika gereza hilo na kuzungumza na Lema. Baada ya mazungumzo yao, Sumaye alisema amefanya hivyo leo kwa kuwa tangu mbunge huyo alipokamatwa na kuweka gerezani alikuwa hajaonana naye.
Alisema afya ya Lema ni nzuri na hajasononeshwa na kwamba amemtaka kuendelea kuwa imara kwani yanayomkabili yatapita.

Source: Mwananchi
ZeroDegree.
Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema akumbukwa akiwa gerezani.
Reviewed by Zero Degree
on
1/01/2017 05:25:00 PM
Rating: