Loading...

Zaidi ya vituo 100 vya Elimu ya Watu Wazima [QT] viko hatarini kufutiwa usajili

Vituo zaidi ya 155 kati ya 337 vya watu binafsi, vinavyotoa elimu ya sekondari kwa vijana na watu wazima kwa kutumia mfumo usio rasmi kupitia Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima nchini (QT). Viko hatarini kufutiwa usajili kwa kukiuka taratibu ikiwemo kutofuata muongozo wa usajili na uendeshaji wa elimu ya sekondari kupitia mfumo usio rasmi.

Hayo yamesemwa leo na Naibu Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, Dkt. Kassim Mhuka wakati akizungumza na waandishi wa habari Februari 17, 2017 jijini Dar es Salaam.

Kufuatia ongezeko la vituo hivyo, Mhuka amewatahadharisha wanafunzi na wazazi kutowapeleka wanafunzi katika vituo visivyosajiriwa au kufuata taratibu husika, huku akiwataka wamiliki wa vituo hivyo kufuata taratibu.

“Napenda kuwakumbusha wamiliki wa vituo hivyo nchini nzima, kufuata muongozo wa usajili na uendeshaji wa elimu ya sekondari kupitia mfumo usio rasmi. Pia tuna watahadharisha wanafunzi wanaosoma katika vituo hivyo kujua kwamba watakosa vitu muhimu ikiwemo kukosa nafasi ya kujiunga kidato cha tano katika shule za serikali au kukosa vyeti vya elimu,” amesema.

Aidha, amesema hadi sasa kuna vituo vya QT zaidi 420 ambapo vya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima viko 83 wakati vya watu binafsi vikiwa 337.

Hata hivyo, Mkuu wa Idara ya Elimu Masafa wa Taasisi hiyo, amesema kwa mujibu wa takwimu iliyofanywa na Shirika la Elimu Duniani (UNESCO) mwaka 2015 inaonyesha kuwa zaidi ya vijana na watu wazima milioni 5 wako nje ya shule. Pia asilimia 50 ya wanafunzi hawaendelei na masomo ya sekondari kwa sababu mbalimbali.

Source: DewjiBlog
Zaidi ya vituo 100 vya Elimu ya Watu Wazima [QT] viko hatarini kufutiwa usajili Zaidi ya vituo 100 vya Elimu ya Watu Wazima [QT] viko hatarini kufutiwa usajili Reviewed by Zero Degree on 2/17/2017 11:47:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.