Jinsi Gwajima na mdogo wake walivyopishana kauli juu ya RC Makonda na vita dhidi ya dawa za kulevya
Baada ya Askofu Josephat Gwajima kutumia zaidi ya wiki tatu kuzungumzia suala la dawa za kulevya na elimu ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa madai kuwa ametumia cheti cha mtu, ndugu yake kiongozi huyo wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kumshambulia akimtaka aache mamlaka husika zifanye kazi yake.
Mwanasheria Methusela Gwajima ambaye ni mdogo wake Askofu Gwajima akizungumza na waandishi wa habari leo amehoji, kwanini suala la elimu ya Makonda limeibuliwa wakati huu ambapo amevalia njuga suala la vita dhidi ya dawa za kulevya.
Mwanasheria huyo ametahadharisha kuwa kama vita hii dhidi ya dawa za kulevya itashindwa, huenda asiibuke mtu mwingine mwenye ujasiri kama Makonda kwa sababu kila mmoja atakuwa anahofia kufanyiwa kama alivyofanyiwa Makonda. Na haya yatakapotokea basi wahusika wa biashara ya dawa za kulevya ndio watakuwa wameshinda.
Wakati huo huo, amemshambulia kaka yake kwa kugeuza suala la dawa za kulevya na elimu ya makonda kuwa sehemu ya mahubiri kanisani kwake.
Mwanasheria Methusela amesema ni lazima watanzania wajiulize ni kundi gani lililopo nyuma ya Askofu Gwajima ambalo ndilo linamsukuma kuendelea kumshambulia Mkuu wa Mkoa na kusababisha kuachwa kwa ajenda ya msingi.
"Watu hawa wanaozungumzia elimu ya Makonda walikuwa wapi? Tangu akiwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni hawakusema chochote ila amegusa dawa za kulevya ndio wameibuka na kuanza kumshambulia?"
Methusela amesema hamaanishi kuwa mabaya ya Makonda yasinguzumzwe, lakini kwanini yamekuja wakati huu?
"Kwanini wanataka kutuhamisha kwenye ajenda yetu iliyopo mezani?. Yani sasa Watanzania tumehamishwa tukaacha kujadili suala la dawa za kulevya na kwenda kujadili cheti cha mtu." amesema Methusela.
Mwanasheria huyo ametahadharisha kuwa kama vita hii dhidi ya dawa za kulevya itashindwa, huenda asiibuke mtu mwingine mwenye ujasiri kama Makonda kwa sababu kila mmoja atakuwa anahofia kufanyiwa kama alivyofanyiwa Makonda. Na haya yatakapotokea basi wahusika wa biashara ya dawa za kulevya ndio watakuwa wameshinda.
Wakati huo huo, amemshambulia kaka yake kwa kugeuza suala la dawa za kulevya na elimu ya makonda kuwa sehemu ya mahubiri kanisani kwake.
“Wewe umeshatuhumiwa, umeitwa Polisi, hivi kwanini usisubiri uchunguzwe? Kama wewe huhusiki si utaambiwa basi. Wameitwa watu wengi, wameitikia wito, kwanini sasa yeye amegeuza kuwa ajenda? Mbaya zaidi imekuwa ni ajenda kanisani. Kwa hiyo kanisa limegeuzwa kuwa kijiwe cha siasa na watanzania wamekaa kimya hawasemi,”alieleza Methusela
"Kama Gwajima anadhani kuwa ameonewa aende mahakamani badala ya kukaa na kulalamika. Kwanini basi anakwepa mahakama na kufanya kanisa ndio sehemu ya kuzungumzia, kila Jumapili ni Makonda, Makonda, Makonda, vyeti, vyeti" amehoji Methusela.
Mwanasheria Methusela amesema ni lazima watanzania wajiulize ni kundi gani lililopo nyuma ya Askofu Gwajima ambalo ndilo linamsukuma kuendelea kumshambulia Mkuu wa Mkoa na kusababisha kuachwa kwa ajenda ya msingi.
Jinsi Gwajima na mdogo wake walivyopishana kauli juu ya RC Makonda na vita dhidi ya dawa za kulevya
Reviewed by Zero Degree
on
3/10/2017 05:34:00 PM
Rating: