Loading...

Jinsi kocha wa zamani wa Simba SC anavyozidi kutamba nchini Ghana

KOCHA wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic, anazidi kuonyesha ubora wake nchini Ghana akiwa na kikosi chake cha Asante Kotoko, kutokana na kutoa dozi kwa kila timu inayokatiza mbele yake.

Katika msimamo wa ligi hiyo kikosi hicho cha Loga kinashika nafasi ya pili kikiwa na pointi 10 na hii ni baada ya mwishoni mwa wiki iliyopita kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Elmina Sharks.

Katika michezo minne ambayo wameshacheza mpaka sasa hawajapoteza mchezo wowote, kwani wameshinda mitatu na kutoka sare mmoja na kama watashinda mchezo wao wa kiporo wanaweza kupanda kileleni.
Loga alisema malengo yake msimu huu ni kuhakikisha kikosi chake kinatwaa vikombe vyote vilivyoko mbele yao.

“Nadhani huu ni mwanzo mzuri kwani matokeo yanaonyesha kuwa tuko bora, ninachokiwaza kwa sasa ni kuhakikisha tunashinda kila kikombe na hilo linawezekana kutokana na uimara wa vijana wangu,” alisema.
Jinsi kocha wa zamani wa Simba SC anavyozidi kutamba nchini Ghana Jinsi kocha wa zamani wa Simba SC anavyozidi kutamba nchini Ghana Reviewed by Zero Degree on 3/08/2017 12:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.