Loading...

Jose Mourinho kashaanza kuuhofia uwanja kabla ya pambano la EUROPA ligi huko Russia

Kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho hajafurahishwa kabisa na hali ya uwanja utakaotumika leo katika mechi yao ya hatua ya 16 bora Europa ligi dhidi ya Rostov huko nchini Russia.

Rostov ambayo ipo nafasi ya 5 katika ligi kuu ya Russia inatumia uwanja wa Olimp-2 uliojengwa mwaka 1930 ukiwa na uwezo wa kuchukua watu takribani 15,000.


Mourinho hajafurahishwa na uwanja huo ambao umeonekana kuwa na viraka vikubwa ambavyo havina nyasi.

“Ni vigumu kwangu kuamini tunaenda kucheza katika huo uwanja kama mnaweza kuita ni uwanja” amesema Mourinho.
Jose Mourinho kashaanza kuuhofia uwanja kabla ya pambano la EUROPA ligi huko Russia Jose Mourinho kashaanza kuuhofia uwanja kabla ya pambano la EUROPA ligi huko Russia Reviewed by Zero Degree on 3/09/2017 01:38:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.