Loading...

Mchakato wa kuhakiki taarifa za wastaafu kuwafikia wahusika hadi vitandani

Uhakiki wa wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango.
UHAKIKI wa wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango wameshindwa kufika katika viwanja vya Karimjee na Mwalimu Nyerere (Sabasaba) jijini Dar es Salaam kwa ajili ya uhakiki wa nyaraka.

Mpango huo umekuja baada ya Mkaguzi Mkuu wa Ndani wa Serikali, Mohamed Mtonga kutoa wito kwa wastaafu walio wagonjwa kutoa namba za simu na majina yao ili waweze kuhakikiwa hospitalini au nyumbani waliko.

Mtonga alitoa wito huo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya zoezi la uhakiki wa taarifa za wastaafu wanaolipwa pensheni na Wizara ya Fedha na Mipango.

Zoezi hilo linalofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia jana, litakamilika Ijumaa.

“Kwa sasa ninavyozungumza zoezi hili liko kwenye hatua ya mwisho katika Mkoa wa Dar es Salaam," alisema Mtonga.

Mtonga alisema wastaafu hao wengi wanaofika kwenye uhakiki walifanya kazi serikalini kabla ya mwaka 1999.

Wastaafu wa miaka hiyo, alisema Mtonga, hawapo katika mifuko ya pensheni na ndiyo ambao wanalipwa pensheni na Serikali, wakiwemo watumishi wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Aidha alisema lengo kubwa la kuhakiki wastaafu hao ni kuboresha daftari la wastaafu ili kusaidia kujua ni kiasi gani cha wastaafu wapo katika kumbukumbu ya daftari la pensheni.

Alisisitiza kuwa wastafu ambao hawatajitokeza watafutwa katika daftari hilo.

Ukaguzi kama huu kwa mara ya mwisho ulifanyika mwaka 2014 kabla ya kuanza tena Oktoba, mwaka jana, alisema.
Mchakato wa kuhakiki taarifa za wastaafu kuwafikia wahusika hadi vitandani Mchakato wa kuhakiki taarifa za wastaafu kuwafikia wahusika hadi vitandani Reviewed by Zero Degree on 3/07/2017 12:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.